Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Na mimi huwa najiuliza wabunge wa Ccm wapo kwenye ubunge tangu Uhuru, wameyafanyie nini majimbo yao! Achilia mbali Halima aliyeongoza kwa miaka 10!
 
Ki ukweli gwaji boy katufanyia makubwa kawe.katuletea hadi kavideo ka ngono wahuni tunakatumia sana kwenye uwakilishi wa chaputa.wasiwasi wetu ni kwamba je tukimpa kula akawa mbunge je atatuletea kavideo kengine je?(in brother k's voice)
 
Tayari jimbo limerudi Ccm, hapa nimekubali kazi nzuri ya intelijensia ya Ccm kumpachika Gwajima awe mgombea wao.
 
Uilyosema Pascal Ni mazuri, lkn pia elimu ya Gwajima unatakiwa ichunguzwe, ana PhD kweli au ni form four.
 
Je maendeleo ya Bongo hayana vyama? ... la hashaaa, serikali ya Bongo hupeleka maendeleo walipo wabunge wa CCM na kutelekeza walipo wabunge wa upinzani, kwa hiyo Kawe awajibike Magufuli na Serikali yake!
... nasema hivi, msimuonee Halima Mdee bali mtumie mizani sahihi kupima wagombea wenu!
😅
👊 ✌️✌️✌️💥
 
Kaka kwanza pole kwa yanayokusibu kiafya sijui ni uzee au unaumwa manake nimekuona juzi kwenye maonyesho ya vyuo vikuu hakika "umeisha" kama ni njaa basi haya uliyoyaandika hapa ni matokeo ya njaa kwani sote tunamfahamu Gwajima anavyojua kuwatumia waandishi wenye njaa sijasema makanjanja kwani wewe sio kanjanja tunakufahamu kitambo sijui "umekula maharage ya wapi" msemo wa Gwajima.

Pili inaonekana umepoteza weredi na umakini wako uliokuwa nao siku za nyuma katika kuelewa na kupambanua wajibu na kazi za Mbunge (Sijui ndio njaa yenyewe) .Kukumbusha tu kazi mojawapo za Mbunge ni pamoja na kuwasilisha matatizo ya wananchi wanaomzunguka Serikalini kupitia bungeni ili yaweze kutatuliwa kupitia kodi zetu tunazolipa. Halima ni kati ya wabunge wachache saana Tanzania (wasiozidi kumi) aliyejizolea sifa kem kem kwa kuwakilisha matatizo si tu ya Kawe bali ya nchi nzima na ndio maana anafahamika nchi nzima kwa uwakilishi bora na uliotukuka bungeni tofauti na Gwajima anayefahamika kuwa ni kati ya wale watumishi "wajanja wajanja" waliojilimbikizia mali nyingi kupitia kuwatapeli wananchi kwa kupitia sadaka lakini vile vile pia hivi karibuni amejizolea sifa nchi nzima kama mchungaji "anayetafuna" kondoo wake na kupewa jina maarufu la Gwaji boy. Tunamshukuru Mungu kwa kumvua nguo kupitia ugonvi wake na Bashite

Kazi nyingine ya Mbunge ni kuzuia na kupigia kelele mali za umma zisifuje au kukwapuliwa na mafisadi. Ebu nikuulize swali Pascal wa zamani (sio wa sasa). Hivi jiulize kama Gwajiboy ndio angekuwa mbunge wa Kawe kwa miaka kumi iliyopita hali ingekuwaje pale Kawe kwa sasa? je zingekuwa zimejengwa barabara za lami kule Goba,madale,makongo? Hivi kweli umejisahaurisha kwamba ni jinsi gani mafisadi wengi wanavyoogopa kupiga "deals" pale Kawe kwa sababu ya uwepo wa Halima?

Naomba umfikishie salamu yule Paschal makini wa zamani tunayemfahamu, Pascal yule aliyesababisha kupigwa marufuku "Press conferences" zoote na JPM kutokana na swali gumu alilomuuliza wakati anaingia madarakani wakati akitangaza baraza lake la mawaziri.

Mwisho wana Kawe wanampenda saana Halima. Isitoshe Gwajiboy alishatangaza kitambo kuwa yeye ni wa juu zaidi na hawezi "kujishusha" kwa kugombea vyeo vya chini kama ubunge au Urais wa nchi sasa sijui amakula maharage ya wapi kwa kuamua "kulamba matapishi yake"!
 
Wote ni hovyo tu; Mdee hastahili kuwamo Bungeni tena kwani badala ya kusaidia mstakhbaliwa Taifa yeye amekuwa ni mtia fujo tu, Gwajima naye ni tapeli tu asiyekuwa na hadhi ya kuwa Bungeni.

Watu wa Kawe wana bahati mbaya sana; ni sawa na kufukuzwa na simba ukajaribu kupanda mti halafu ukakutana na chui huko. Sijui kwa nini Kawe imekuwa na bahati mbaya miaka yote. Alipokuwapo Mlaki naye alikuwa Bomu tu; alipokuja Mdee naye amekuwa bomu tu, sasa sijui itakuwaje huko mbeleni. Lakini Kawe ambayo ni sehemu yenye wasomi wengi na watu wenye uelewa wa hali ya juu sana ndiyo imekuwa na representation mbovu sana Bungeni miaka yote.
 
Wajumbe [emoji1787]
 
Jiwe kafanya nini kwa miaka 5?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anko anko ,tafadhali anko jimbo la kawe nendeni kwa step ,la sivyo mtalipoteza ,usijidanganye kabisa

Ccm kawe inampasuko hamko wamoja ,kata ya msasani na Mikocheni msiziamini
 
Gwajima inabidi kazi ifanyike Sana ili ashinde
 
Mkuu P,kweli kabisa Askofu Gwajima kwa hayo aliyofanya anastahili ubunge,lkn mh Halima mdee yeye ni mbunge wa kitaifa.kwa hoja anazoibua bungeni kwa utawala huu kuwa na bunge bila ya kua na watu Kama kina mdee,chenge litaenda kua bunge la hovyo duniani,mdee ni mtetezi wa wananchi wote ,ccm ni chama kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…