Mafiningo
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 4,435
- 4,662
Kw jinsi jina lako lilivyokubwa hapa jf sijategemea uweke hoja kama hii hapa.Wanabodi,
Mimi ni mkazi wa Kawe, kwa vile sasa tuko kwenye kampeni za uchaguzi, ili tumtendee haki Mbunge wetu aliyemaliza muda wake, Mhe. Halima Mdee, ambaye, baada ya kuwa Mbunge wa Kawe kwa vipindi viwili mfululizo, na sasa anaomba tena tumchague, hivyo nauliza kama kuna mtu yoyote anaweza kutueleza humu, hata jambo moja tuu, Jee Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee, amelifanyia nini jimbo la Kawe katika kipindi chake chote cha miaka 10?, ili tumfanyie assessment kama anastahili jee anastahili kuongezewa miaka mitano mingine, or she did nothing hivyo anastahili apumzishwe?.
Declaration of Interest
Japo mimi Paskali Mayalla kwa sasa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, lakini bandiko hili sio la ukada au propaganda za kampeni za uchaguzi, bali ni bandiko hojaji ya halali na swali la ukweli la mwana Kawe, kuuliza Mhe. Halima Mdee ameifanyia nini Kawe in the past 10 years kustahili kuendelea?.
Rais John Kennedy wa Marekani aliwahi kusema, " usijiulize Marekani imekufanyia nini, bali ujiulize, wewe utaifanyia nini Marekani". Mhe. Halima Mdee ndie Mbunge wetu Kawe kwa kipindi cha miaka 10, naomba kuuliza kwa anayejua, Jee Halima Mdee ameifanyia nini Kawe?.
By the way: Leo nilikuwa mahali nikamsikia Askofu Gwajima, kumbe huyu Askofu ni mdau mkubwa wa maendeleo ya watu wa Kawe kwa kipindi kirefu na ameisha fanya mambo makubwa kwa wana Kawe kama Mwananchi tuu wa kawaida bila hata kujua kuwa kuna siku atakuja kugombea ubunge wa Kawe.
Kumbe Askofu Gwajima baada ya kuhamia Kunduchi Salasala, alikuta kuna tatizo la maji. Kwanza alichimba visima virefu 12 kwenye misikiti ya Salasala na kuwapatia maji Waislamu, kisha akanunua pump ya mamilioni kutoka Ujerumani, akanunua mabomba na mita za maji na kusambaza maji kwa kaya 250 za majirani wake wanaomzunguka, sasa wanapata maji safi na salama!.
Askofu Gwajima tayari ameisha saidia magari 7 ya ambulance za wagonjwa kwa hospitali mbalimbali, na kuahidi atazipatia magari ya wagonjwa hospitali za Kawe na Kinondoni.
Gwajima amesema, kazi ya kuwaletea maendeleo Watanzania sio kazi ya serikali pekee, ni kazi ya wananchi kwa kushirikiana na serikali, hivyo hapo alipo, tayari ameagiza tinga tinga la kuchonga barabara na malori mawili ya tipper, ambapo barabara zote za Kawe na Kinondoni zitachongwa, vijana wa Kawe watapatiwa ajira za kuchimba mitaro ya maji, hivyo kama ni serikali, itabaki kazi ya kuziwekea tuu lami!.
Mwana Kawe yoyote akiyasikia haya Askofu Gwajima aliyoyafanya Kawe, kabla hata hajawa Mbunge, ukilinganisha na alichofanya Mhe. Halima Mdee kipindi chake chote cha miaka yake 10!, ukiambiwa umchague mmoja kati ya hawa wawili, utamchagua nani?.
Utakubaliana na mimi kuuliza, Jee is it, it's high time, tumshukuru Mhe Halima Mdee kwa utumishi wake wa miaka 10 Kawe?, na tumuage kwa upendo, heshima na taadhima kwa kumwambia, Bye Bye Mhe. Halima Mdee Kawe, asante sana kwa utumishi wako wa miaka 10 Kawe?, na Jee sasa tumkaribishe Askofu Dr. Josephat Gwajima kwa kumwambia, "karibu, Kawe Askofu Gwajima ili kuikamilisha kazi nzuri ulioshaanza kuitenda kabla hata hujawa Mbunge?.
Nauliza tuu!.
Paskali
Gwajima anakusanya sadaka (fedha + mali) kutoka kwa wanannci kisha amechimba kisima kaweka na mita ili afanye biashara ya maji.
Serikali inakusanya kodi(fedha+mali) kutoka kwa wanannchi, basi na iweke miradi ya kusaidia wanannchi hapo Kawe. Kama hakuna kitu basi tuikosoe serikali na kisha tuikumbushe kuwajibika kwa wanannchi ambao inaenda kukusanya kodi kwao.
Halima anakusanya fedha zipi kutoka kwa wanannchi ?
Hii hoja haujaiweka vizuri ili iwe hoja hasa, nadhani ushabiki wa vyama umekukengesha.