Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Wanabodi,

Mimi ni mkazi wa Kawe, kwa vile sasa tuko kwenye kampeni za uchaguzi, ili tumtendee haki Mbunge wetu aliyemaliza muda wake, Mhe. Halima Mdee, ambaye, baada ya kuwa Mbunge wa Kawe kwa vipindi viwili mfululizo, na sasa anaomba tena tumchague, hivyo nauliza kama kuna mtu yoyote anaweza kutueleza humu, hata jambo moja tuu, Jee Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee, amelifanyia nini jimbo la Kawe katika kipindi chake chote cha miaka 10?, ili tumfanyie assessment kama anastahili jee anastahili kuongezewa miaka mitano mingine, or she did nothing hivyo anastahili apumzishwe?

Declaration of Interest
Japo mimi Paskali Mayalla kwa sasa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, lakini bandiko hili sio la ukada au propaganda za kampeni za uchaguzi, bali ni bandiko hojaji ya halali na swali la ukweli la mwana Kawe, kuuliza Mhe. Halima Mdee ameifanyia nini Kawe in the past 10 years kustahili kuendelea?

Rais John Kennedy wa Marekani aliwahi kusema, " usijiulize Marekani imekufanyia nini, bali ujiulize, wewe utaifanyia nini Marekani". Mhe. Halima Mdee ndie Mbunge wetu Kawe kwa kipindi cha miaka 10, naomba kuuliza kwa anayejua, Jee Halima Mdee ameifanyia nini Kawe?.

Najua kuna watu watasema kazi ya kuleta maendeleo ni kazi ya serikali, kazi ya Mbunge ni kuisimamia serikali, tumekuwa tukishuhudia wabunge wa majimbo mengine wakipigamia majimbo yao Bungeni, Jee Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee, aliwahi kupigania nini cha maendeleo ya Kawe?. Kama kuna anayejua humu, atuambie hata kitu kimoja tuu cha Kawe ambacho Halima Mdee alikipigania?.

Kuna zile fedha za Mfuko wa Jimbo. Jee kuna mwana Kawe yoyote, aliwahi kumshuhudia Mbunge wetu Mhe Halima Mdee akija eneo lolote la Kawe na kuchangia shughuli zozote za maendeleo kupitia fedha za mfuko wa Jimbo?.

By the way: Leo nilikuwa mahali nikamsikia Askofu Gwajima, kumbe huyu Askofu ni mdau mkubwa wa maendeleo ya watu wa Kawe kwa kipindi kirefu na ameisha fanya mambo makubwa kwa wana Kawe kama Mwananchi tuu wa kawaida bila hata kujua kuwa kuna siku atakuja kugombea ubunge wa Kawe.

Kumbe Askofu Gwajima baada ya kuhamia Kunduchi Salasala, alikuta kuna tatizo la maji. Na kufuatia eneo la Kunduchi ni eneo la pembezoni mwa bahari, ukichimba visima vifupi, utapata maji ya chumvi, Hivyo Askofu Gwajima kwanza alichimba visima virefu 12 vya mita 300 kwenda chini ili kupata maji safi na salama kwa ajili ya wana Kawe!. Miongoni mwa wafaidika wa visima hivyo virefu, kwenye misikiti 7 ya Salasala hivyo kuwapatia maji Waislamu, maji ya kutawadha kabla ya kuswali.

Kisha akayatafuta maji ya Dawasco, yanapita mbali, akaomba kibali Dawasco, akanunua manomba kama ya Dawaco ya kusambaza maji, akayatandika kuwatumia mafundi wa Dawasco, anunua pump ya mamilioni kutoka Ujerumani, akanunua mita za maji kama za Dawasco na kusambaza maji kwa kaya 250 za majirani wake wanaomzunguka, sasa wanapata maji safi na salama!.

Askofu Gwajima tayari ameisha saidia magari 7 ya ambulance za wagonjwa kwa hospitali mbalimbali, na kuahidi atazipatia magari ya wagonjwa hospitali za Kawe na Kinondoni.

Gwajima amesema, kazi ya kuwaletea maendeleo Watanzania sio kazi ya serikali pekee, ni kazi ya wananchi kwa kushirikiana na serikali, hivyo hapo alipo, tayari ameagiza tinga tinga la kuchonga barabara na malori mawili ya tipper, ambapo barabara zote za Kawe na Kinondoni zitachongwa, vijana wa Kawe watapatiwa ajira za kuchimba mitaro ya maji, hivyo kama ni serikali, itabaki kazi ya kuziwekea tuu lami!.

Mwana Kawe yoyote akiyasikia haya Askofu Gwajima aliyoyafanya Kawe, kabla hata hajawa Mbunge, ukilinganisha na alichofanya Mhe. Halima Mdee kipindi chake chote cha miaka yake 10!, ukiambiwa umchague mmoja kati ya hawa wawili, utamchagua nani?.

Utakubaliana na mimi kuuliza, Jee is it, it's high time, tumshukuru Mhe Halima Mdee kwa utumishi wake wa miaka 10 Kawe?, na tumuage kwa upendo, heshima na taadhima kwa kumwambia, Bye Bye Mhe. Halima Mdee Kawe, asante sana kwa utumishi wako wa miaka 10 Kawe?, na Jee sasa tumkaribishe Askofu Dr. Josephat Gwajima kwa kumwambia, "karibu, Kawe Askofu Gwajima ili kuikamilisha kazi nzuri ulioshaanza kuitenda kabla hata hujawa Mbunge?.

Kama kuna mtu yoyote ana video clip yoyote ya Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee akishiriki shughuli yoyote ya maendeleo Kawe, naomba aielete ili angalau tumuone!
Shuhudia mwana Kawe huyu anavyojituma kwenye kuleta maendeleo

View attachment 1558915

Nauliza tuu!.

Paskali
kweli serikali za majimbo zinahitajika ili watz wajue majukumu ya mwakilishi na mtawala, kama hadi msomi kama wewe unauliza mbunge amefanya nini jimboni!!!!??? Kwani alipewa utawala au uwakilishi kodi anakusanya yeye? Nani anayepanga matumizi ya hela jimboni. Katiba mpya muhimu watz hatujielewi nani anawajibika kutatua matatizo yetu
 
Je Mkuu tukisema kwamba mnakubaliana kwenda bungeni kwa gharama zozote ili kupitisha sheria ya misikiti kugeuzwa sunday school tutakuwa tunakosea? Sihitaji kusema sana kama "hamtotumia bunge tena kutusi maaskofu wenye heshima zao kwa maana mtakuwa na kinga!!"
 
Mnaodai serikali ndio haipeleki hela kwenye majimbo ya upinzani

muwe hata mnaangalia majimbo mengine ya upinzani hali iko vipi

nendeni mikumi huko kwa bwana Joseph muone mabalaa yake halafu

ndio muongee nje nje nje zenu,Hoja hamjibu mpo kumshambulia paschal

kaleta mjadala watu mseme yupi n yupi hata kama n kampeni sawa mkosoeni

kulingana na thread inavyotaka sio kuleta ujuaji mwingi,ki ufupi Halima this time Aje kitaani tu.
 
Naona umeamua kufanya kampeni kwa Gwajima. Sasa kwa taarifa yako ni kuwa Kunduchi ina maji ya Dawasco na bahati mbaya sana mimi ni mtaalam kwa hiyo maji ya kisima cha chini Kunduchi ni maji ya chumvi sana hivyo naamini hayapo kwa matumizi sasa.

Halafu kutoa pump za maji ya Kisima cha chini Ujerumani nayo ni ishu? Vile vi pamp vipo hata Kariakoo vimejaa tele!

Mkuu emb kuwa na adabu na kichwa chako na ujue kuwa unaleta mada zako kwa wataalam!
Mkuu tatizo la "maccm" wengi ni kuamini katika udini na ukabila.
HAWATUPANI NDIO MAANA ZILE KAULI "Huyu MWENZETU huyu KIBARAKA zingaliko hata leo!!
Hivi aliyesema hapeleki maendeleo kwenye upinzani ni nani? Hivi hali ya Ilala na Kawe ni ipi?
 
wananchi mlioko Kawe mnaulizwa Mdee kafanya nini jimboni kwake?
Hili swali bado halijajibiwa pamoja na uzi umefika page ya 9
Mimi ni mkazi wa Kawe sijawahi kumuona Mbunge wa jimbo hili kwa miaka 6 iliyopita pamoja na kuwa mhudhuriaji mzuri wa mikutano ya maendeleo huku upande wa Bunju. Mtu pekee nilemuona akishughulikia matatizo ya wananchi hasa ya ardhi alikuwa Waziri Lukuvi. Sijui Halima Mdee anafeli wapi hatumuoni kabisa jimboni ila kwenye vyombo vya habari akipambana na dola na kukwaruzana na spika.
 
Gwajima alishasema hawezi kutaka ubunge wala urais kwani huko yeye kama mtumishi wa Mungu itakuwa ni kujishusha hadhi.

Urais na ubunge alisema ni kuwatumikia wanadamu.

Gwajima alirekebisha lini maneno yake hayo? Huu si ndiyo ule uaskofu uchwara?
Uko sahihi mkuu,huyu Pascal badala ya kumjadili mgombea wao kigeugeu unamrukia Halima hivi wamelogwa??Halafu mccm analeta mada hapa tumfanyie assessment Halima kwa lipi watamfanyia fair??wazinzi na wakabila hawawafanyii assessment mimi nadhani huyo na hao waliompitisha mzinifu ndio wakufanyiwa assessment maana huyo mgombea wao hata wajumbe walimkataa vitu vya ajabu kabisa hivi.
 
Jibu hoja ,acha ufala ,Halima Mdee kaifanyia nini Kawe ndani ya miaka kumi akiwa mwakilishi wa jimbo ?
1....
2.....
3.....
4......
5.......


Ulitaka ajenge uwanja wa ndege kama huyo mvutabangi wako wa Chato?????

Baki na huyo Askjofu wako wa mivutu
 
wananchi mlioko Kawe mnaulizwa Mdee kafanya nini jimboni kwake?
Hili swali bado halijajibiwa pamoja na uzi umefika page ya 9


Endelea kumpigia debe Mlaji mivutu ,

Kwani CCM imefanya kitu gani cha maana miaka zaidi ya 50 sasa
 
Kumchagua mtu kwa vile ana pesa za kuchonga barabara ni kujidhalilisha maana mtakuwa mmenunuliwa. Chagueni mtu atakayewapigania ili mtendewe haki kutokana na kodi mnayolipa. Maendeleo sio fadhila, ni haki yenu.
Amandla...
Pasikali ameshakuwa mwana siasa (ndio maana kaingia mchakato). Hapa anaonyesha uelewa wake wa jukumu la mbunge. Hawa ndio wanasema maendeleo hayana chama, halafu hapo hapo wanasema ukitaka maendeleo chagua CCM. Hata aseme je hawezi tena kuwa neutral au anafikiri sisi ni mapoyoyo.
 
Kwa nini usitwambie ccm imefanya nini Kawe kwa miaka 60 ikikusanya kodi zao?
Huyu Mayala kweli Mayala, njaa imempanda kichwani
 
Pasikali ameshakuwa mwana siasa (ndio maana kaingia mchakato). Hapa anaonyesha uelewa wake wa jukumu la mbunge. Hawa ndio wanasema maendeleo hayana chama, halafu hapo hapo wanasema ukitaka maendeleo chagua CCM. Hata aseme je hawezi tena kuwa neutral au anafikiri sisi ni mapoyoyo.
Hapo alipo njaa imeshapanda kichwani, hajitambui tena kawa Mayala ( njaa) kwelikweli
 
Back
Top Bottom