SOVIET UNION
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 509
- 1,391
Kuna gari 400 plus za halmashauri zote Tanzania. Kuna halmashauri unakuta ina gari 3: Mkurugenzi gari lake na watumishi wengine gari zao. Kwa ujumla, Arusha kuna gari 500 na zaidi za halmashauri Tanzania nzima.
Sasa chukulia kwa mfano halmashauri za Mkoa wa Lindi wakaamua kuungana na Mtwara wakachukua Yutong moja safi kabisa wakaja nayo Arusha. Je, jua halitazama? Arusha wakifika wanaweza kodi tax za kuwapeleka mkutanoni na kuwarudisha hotelini, lakini kwa taifa ambalo kuanzia Mkuu hadi Chini ni watu wa matumizi, hili haliwezekani.
Mzigo unaishia kwa kuongeza tozo kwa raia ili kuhudumia halmashauri kwa sababu ya matumizi ya anasa. Ukiwakuta juu ya majukwaa wanalia lilio cha mamba kwa shida za wananchi.
Arusha kwa leo, ukikata kona unakutana na gari za halmashauri mara Kibondo, mara Kishapu, mara Manyoni. Hapo bado, ma V8 ya wakurugenzi ambayo hayana maandishi yoyote.
Na hapo anaye fungua mkutano utasikia anawaambia waongeze juhudi kwenye kuhudumia raia. Huku nje ya ukumbi, kukiwa na magari 400 plus, na hapo hapo vijijini kumejaa project zinazoendeshwa kwa michango ya wananchi wanaochangishwa kwa nguvu na wala sio kwa hiari yao.
Hawa ndio watawala tunangoja watufikishe uchumi sawa na Vietnam au Thailand au Malaysia.
Ukiwakuta viongozi wakuu kama Rais, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wanavyolia, utajua wako serious na kuinua hali za maisha ya wananchi, kumbe ni hadaa tupu. Hakuna kiongozi ndani ya CCM yuko interested kuondoa umaskini.