sawa leo mkuuTunasubr mrejesho wa hiko kifurush cha 50k Halotel (kifahari) kwenye lain Za M2M wanazo sema ni unlimited feedback yako ni muhim sana je baada ya hzo 24GB speed inapungua au haipungui ..? na kama inapungua inafka ngap yan Mbps ngap
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sawa leo mkuuTunasubr mrejesho wa hiko kifurush cha 50k Halotel (kifahari) kwenye lain Za M2M wanazo sema ni unlimited feedback yako ni muhim sana je baada ya hzo 24GB speed inapungua au haipungui ..? na kama inapungua inafka ngap yan Mbps ngap
Speed inashuka mpaka 3mbps to 15, depends na eneo & muda. Mfano kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 5 usiku speed inachezea kati ya 3-7.Tunasubr mrejesho wa hiko kifurush cha 50k Halotel (kifahari) kwenye lain Za M2M wanazo sema ni unlimited feedback yako ni muhim sana je baada ya hzo 24GB speed inapungua au haipungui ..? na kama inapungua inafka ngap yan Mbps ngap
Blaza kwa hii feedback Mungu akubariki umongea kila kitu nilchokua nataka kujua asante sana 🤝🔥kuhusu kifurushi cha Halotel M2M, huduma hii ina faida na hasara zake kulingana na aina ya matumizi yako. Kulingana na matumizi yangu kwa mwezi, hapa kuna maoni yangu:
1. Je ni unlimited kweli?
Kifurushi hiki sio "unlimited" kwa maana ya kupata internet bila kikomo kwa kasi ya juu kila wakati. Ni "unlimited" kwa maana ya kwamba hautakatazwa kabisa kutumia internet ndani ya siku 30, lakini kasi itapunguzwa baada ya kufikia kikomo fulani cha matumizi (GB 350).
2. Zikihisha hizo GB 25 za mwanzo, speed inakuaje?
Baada ya kutumia GB 25 za mwanzo kwa kasi ya juu (15-30 Mbps), kasi itapunguzwa kati ya 3-15 Mbps hadi utakapofikia GB 350. Baada ya hapo, kasi inaweza kushuka hadi 500 kbps - 3 Mbps, kulingana na kiasi cha data unayotumia.
3. Kwa watumiaji wa kudownload big files (wale wazee wa kushusha files), kinawafaa?
Kifurushi hiki si rafiki sana kwa wale wanaodownload files kubwa sana mara kwa mara. Kasi itapunguzwa kadri unavyotumia data zaidi, na hii inaweza kuathiri sana ufanisi wa kushusha files kubwa.
4. Inafaa kwa wanaolenga kuunganishia watu wengi kwa matumizi ya kwenye jumuia?
Kwa matumizi ya kuunganishia watu wengi, kifurushi hiki si chaguo bora. Kwa kawaida, itafaa zaidi kwa watu wachache (hadi watu 5), lakini zaidi ya hapo, kasi itashuka sana na kufanya matumizi kuwa magumu kwa wote.
5. Vigezo na namna ya kujiunga na huduma?
Unahitaji kutembelea duka la Halotel ili kujiunga na huduma hii. Utahitaji kuwa na TIN namba na leseni, na unaweza kununua router kwa bei ya kati ya 100k na 150k. Pia, kuna njia zisizo rasmi ambapo unaweza kusaidiwa kuunganishwa na huduma kwa posho ndogo.
Ni muhimu kufahamu kwamba huduma za internet zinaweza kutofautiana kulingana na eneo na eneo ulipo. Pia, watoa huduma wanaweza kubadilisha sera zao wakati wowote, hivyo ni muhimu kuwa na ufahamu wa hali ya sasa na kutegemea taarifa mpya kila mara.
Nawasilisha kama kunaswali au nyongeza uliza
Uatumia kwenye router au simu kawaida? kukatika na kurudi kwa mtandao ni kweli na nishida ipo ata kwenye line zao za kawaida Halotel mtandao haupo stable, pia hapo nimesahau kuelezea speed ya UPLOAD nimeongelea Download tu, Bora umenikumbusha kuwa baada ya kama gb 100 hivi kuisha Upload huwa wanazima kabisa yaani ni 0.1-1 mbps kwaiyo kwa online calls na hishu kama za skype, na wale wa kupload files to online, kifurushi hiki sio rafiki kwenu.Natumia hyo lkn hamna kitu. Speed yao iko slow sana alaf inakata muda wowote yani i akuja na kuondoka. Kama una kazipengine kama interview ya online usijaribu ndugu yangu. Hii naisema kama mtumiaji mwez wa pili mfululizo
Mkuu nilianza kwa kutumia router nilivyoona mtandao hauko stable nikarudi kutumia simu nikdhani labda router ndo ina shida lkn tatizo likabaki kuwa lile lile nikaamua kudi tena kwenye router lkn shida bado ileileUatumia kwenye router au simu kawaida? kukatika na kurudi kwa mtandao ni kweli pia hapo nimesahau kuelezea speed ya UPLOAD nimeongelea Download tu, Bora umenikumbusha Upload huwa wanazima kamisa yaani ni 0.1-1 mbps kwaiyo kwa online calls na hishu kama za skype, na wale wa kupload files to online msijaribu kabisa hichi kifurushi sio chenu tafuteni package nyingine.
Shida hiyo unaipata baada ya kuisha hizo gbs 25? , rudia kusoma hapo juu kuna kitu wanafanya speed throttling, yaani kuna limit ya jumla kwa mwezi na limit ya siku, ukifikisha kiwango cha mwisho kwa siku wanakushushia speed kwa siku iyo.Mkuu nilianza kwa kutumia router nilivyoona mtandao hauko stable nikarudi kutumia simu nikdhani labda router ndo ina shida lkn tatizo likabaki kuwa lile lile nikaamua kudi tena kwenye router lkn shida bado ileile
OnjaKuna mtu kaniambia kuna halotel unlimited ila ikipita gb 24 inapungua spidi, je hiyo spidi ipoje baada ya 24gb.
Mwisho la kuzingatia na ni muhimu kifurushi hicho hakina mkataba wowote unaoingia nao na kampuni husika, mfano wakati najisajili na huduma ya Tigo POSTPAID niliingia mkataba wa 2 year's moja ya faida ya mkataba huo ni kuwa terms za mkataba hazito badilika mpaka muda utakapo kwisha.
Kwaiyo ikitokea kifurushi kikashuka bei mimi bado nitaendelea kupata huduma kwa ileile bei ya juu, na vikipanda bei bado nitaendelea kupata kwa bei ileile ndogo.
Tuje kwa hao halotel hakuna mkataba wowote means muda wowote wakati wowote wanaweza kufuta au ata kubadilisha sera yeyote na pigine kuongeza bei pasipo kuhoji lolote lile.
Ushauri wangu kwa wale wenye huduma zenye uwakika kutoka kwenye makampuni mengine wasiache kutumia huduma zao hizo then wakimbilie hii huduma kisa kitonga cha 50k watakuja kukwama siku moja, hii tunatumia kama BACKUP na sio kutegemea kuwa ni huduma ya uwakika
kwel kabisa wamepunguza kwa kiwango kikubwa nime experience hiloNEW UPDATES: Halotel wamepunguza kikomo cha gbs kutoka Gb 350 hadi Gb 100 , baada ya kumaliza GB 100 hizo, kasi ya intaneti imepunguzwa kutoka 3Mbps hadi 0.4Mbps. , Kwa mabadiliko haya, kifurushi hiki kimepoteza sifa ya kuitwa "unlimited" kabisa na kwa wale waliokuwa wanatarajia kujiunga sasa watafakari hilo kwa makini.
Wanahitaji 5G hawa jamaa.NEW UPDATES: Halotel wamepunguza kikomo cha gbs kutoka Gb 350 hadi Gb 100 , baada ya kumaliza GB 100 hizo, kasi ya intaneti imepunguzwa kutoka 3Mbps hadi 0.4Mbps. , Kwa mabadiliko haya, kifurushi hiki kimepoteza sifa ya kuitwa "unlimited" kabisa na kwa wale waliokuwa wanatarajia kujiunga sasa watafakari hilo kwa makini.
kwan shida ipo wap si tuna hama tu 😂😂 wakipoteza wateja akili ikikaa sawa watatuliaWanahitaji 5G hawa jamaa.
4G ngumu mkuu Kuhudumia capacity. Ila kwa 5G rahisi Kuhudumia unlimited. HALOTEL wana fiber nchi nzima, ni minara yao tu ya 4G inawaangusha.kwan shida ipo wap si tuna hama tu 😂😂 wakipoteza wateja akili ikikaa sawa watatulia
Kaka tunaomba mrejesho kutoka kwako....Kama kwa matumizi ya kawaida bado hiyo kasi sio mbaya sana, ila mwisho wa mwezi huu nitaleta mrejesho juu ya uzoefu nilioupata kuhusu hizo laini zao maalum na kifurushi hicho cha unlimited.
Maana nimejiunga tarehe 28/07/2024, hivyo bado siwezi kusema nimeijua vyema huduma hii ipo vipi. Ila kwa watakaotaka kujua hasara na faida za huduma hii, basi nitakuwepo hapa tarehe 29/08/2024, Mungu akipenda, nikitoa ufafanuzi wa mwanzo hadi mwisho kuhusu kifurushi hicho
Mimi pia natumia,Mie natumia halotel ya elf 50 sijawahi kujuta nakuwa youtube kwenye tv vizuri tu
Halo shop ulipoenda wamekudanya ukweli ni kuwa toka tarehe moja wame weka sera mpya ambapo kikomo cha GB kimeshuka kutoka 350 hadi 100, na ukishamaliza hizo gb 100 tena wameshusha speed kutoka 3mbps hadi 0.512mbps kwaiyo kwa speed iyo hakuna kitu utaweza kufanya zaid ya browser.Kaka tunaomba mrejesho kutoka kwako....
Mimi ninatumia unlimited ya halotel mwezi wa 4 .
Ila kwasasa imeshuka sana speed siwezi kufanya kitu kbs...
Leo siku ya nne.
Nimewaambia niliponunua wananiambia halotel wanafanya maintainance hvy tuvumilie sipo peke yangu.😭😭😭