Je, Harmonize alifanya uamuzi sahihi kuuza nyumba zake 3 katika harakati za kujitoa WCB? Wewe ungefanyaje?

Je, Harmonize alifanya uamuzi sahihi kuuza nyumba zake 3 katika harakati za kujitoa WCB? Wewe ungefanyaje?

Aslay habari nyingine ile lakini angalia leo hii, Harmonize ana thamani kubwa maradufu kumlinganisha na Aslay!!! Hata huyo Mario, labda hujamsikiliza vizuri tu au inawezekana tastes zake huzi-feel! But all in all, bado huwezi kumlinganisha Mario na Harmonize ambae kwangu namuona ni kama clone ya Diamond!!

Advantage ya Harmo kwa WCB ni kama aliyokuwa nayo Nandy kwa Clouds! Leo hii watu wanadiriki kumlinganisha Nandy na Ruby; are we serious?! Unamlimganisha vp Nandy na Ruby!! Lakini ukweli wenyewe ndo huo; Nandy ana thamani kubwa kuliko Ruby ingawaje Ruby ana uwezo mkubwa sana kumlinganisha na Nandy!!! Wakati Nandy ni mwanamuziki wa kutenegenezwa, Ruby ni natural born but still she's very far compared to Nandy linapokuja suala la uwezo binafsi!
Msanii wakutengenezaa??

Unamaana gani nandy anapoimba ni sio yeye ni ana kifaa cha kiimbia ndomoni gás au Wakutengeneza vipi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mabasi hawana uhakika na branding strategy zao. Pia maajali nk bus line moja ikichafuka kama ndio hio tu unayo basi umekwisha. Kwa hio wanafanya kama insurance moja ikichafuka na kuanguka nyingine inaokoa jahazi. Asante kuendelea kuchangia mada Bwana Eyce

Ni kweli ila kinachofanyika huwa kina faida zaida ya moja. Mfano leo hii mtu anaichukia clouds kutokana na story za hapa na pale na anaamua kuwa fan wa wasafi bila kujua zote ni za mtu mmoja. So kuna mafaida mengi ingawa hiyo ya kusambaza RISK ni kubwa pia

Pamoja mkuu
 
Msanii wakutengenezaa??

Unamaana gani nandy anapoimba ni sio yeye ni ana kifaa cha kiimbia ndomoni gás au Wakutengeneza vipi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasanii wengi Bongo originally wanakuwa below the average! Inafanyika kazi ya ziada kuwapika hadi kufikia walipo! Wanakuwa hawapo vizuri kwenye sauti, melody na mengine!! Ukimchukulia mtu kama Nandy, kaanza muziki zamani sana lakini bado alikuwa average! Ni hadi Ruby alivyovurugana na Clouds, ndipo Clouds wakahamishia nguvu zao kwa Nandy! Kuna wasanii hadi kesho hadi melody hadi uwatengenezee, ndipo wao wapite mule mule!

Hiyo ni aina ile ya wasanii ambao Majani zamani alikuwa anawatoa nduki mara baada ya kuanza kuingiza voko!
 
Watu wengi hamjui tu hamna kitu chepesi kama kuwa number moja,ila hamna kitu KIGUMU kama kumaintain kuwa number moja kila siku.

Aslay, Darassa hawa washawahi kuwa number moja ila wakashindwa kumaintain,sio kwamba hawana vipaji bali hawana mngt nzuri ya kuwa simamia na kusimamaia kazi zao.

Kwenye kumaintain na connection hapo ndipo WCB wazuri.Kitu kingine WCB wanaweza wakabebana (wakafanyiana induction) wao kwa wao mf tu sasa hivi wana haha kumrudisha Lavalava naamini watafanikiwa.

Mngt ya Harmo ina kazi ya ziada ya kumaintain brand aliyotoka nayo WCB na si kazi ndogo,wakiteleza kidogo tu harmo tutamkosa.
 
Marioo ni average singer ila lyrical genius. Ana kipaji kikubwa sana cha kutunga. Binafsi yangu huwa sisikilizi wimbo kwa sababu upo mainstream ila huyu jamaa wimbo wa inatosha na Raha ndio zilinifanya nimkubali
Huyu mwamba anamkono wa uandishi sio kidogo, kwenye nyimbo zake hua sifuati burudan sana, tungo zake tu..anajua sana kuandika, watu wengi hawamwelew kwasababu mashairi ya maana siku hz sio issue tena....mfumo wa uimbaj wa ki naijeria umetuvuruga mno...lait kama angekua ni kizazi cha 2000-2010 hapo katikat..mashair yake yangedumu milele..huyu mtoto n wakizaz kile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wew wa mkoan huwez elewa.hiv hujui bifu znatengenezwa ili kupiga pesa.hyo ni marketing strategy ,nenda kina tale wakakupe shule,.we hujiuliz wasaf na clouds CEO ni mmoja ila redio ni kama zna bifu,..we hukumwona kusaga anahojiwa na jonijo...wa mkoan buana
Kitendo cha Diamond kukaa kimya..kinaua dhana nzima ya bifu na upigaj pesa..kinaua kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo mkataba ulikua na thamani ya sh ngapi?
Kama katumilia miaka 4 na kabakiza 6 analipa million 500 basis. Mkataba wake ulikua na thamani zaidi ya Billion 1.
Kwa biashara gani inayofanyika kwenye music industry Tanzania mkataba use na thamani hiyo?
Kwa mkataba huo Harmonize alikua anainhizia kampuni zaidi ya 1.5bilion kwa miaka 10.

KAMBA HII AISEE
B1 ni hela ndogo sana mkuu,sasa kama show moja ya msanii kma Harmonize inaingiza zaidi ya M 30,tufanye roughly anafanya show moja kwa mwezi ina maana kwa mwaka 1 nazungumzia sales za zaidi ya M300 hatujapiga miaka 10.seems bado unaiunderestimate hii industry!
 
I wish diamond amsainishe Marioo kijana ana kipaji sana na anaonekana ana juhudi sema anahitaji platform huyu hatahitaji kutumia nguvu nyingi kama aliyotumia kwa Hamo
 
Bila hela hakuna hela. Bila WCB kuwekeza kwake, asingefanikiwa. Hivyo WCB imechangia mafanikio yake kwa kuwekeza kwake kifedha. Tunasema Mungu amtangulie. Lakini kwa sasa anahaha wakati Diamond anachekelea tu. Tatizo alifanya ni kusaini mkataba mbovu unaomuumiza. Na hilo ni kosa alilofanya kipindi hicho lakini linamgharimu sana sasa hivi.
Hivi ilishindikana jamaa kuanza kununua vifaa vyaje kimya kimya i.e vifaa vya studio ya kurecord mziki, kurecord video, na mwisho kua na recording label na bila kusahau kua na online TV i.e Konde TV, kutafuta connection za kufanya matamasha nje ya nchi halafu hapo ndo anajitoa maana kujitoa kama alivyojitoa kimbuzi mbuzi ni risk kubwa walau angelikua na hivyo vitu inakua rahisi hata watu kumsimamia vizuri au anavyo hivyo vyote?
 
Wew wa mkoan huwez elewa.hiv hujui bifu znatengenezwa ili kupiga pesa.hyo ni marketing strategy ,nenda kina tale wakakupe shule,.we hujiuliz wasaf na clouds CEO ni mmoja ila redio ni kama zna bifu,..we hukumwona kusaga anahojiwa na jonijo...wa mkoan buana
WASAFI MEDIA CEO wake ni DIAMOND PLATNUMZ na clouds media CEO wake ni Sebastian maganga hapo kwenye CEO umekosea
 
tatizo mkuu inakuja vipi, unakuta mtu underground, huku akiwa na shauku ya kutka kutoka kimuziki hapo hata angeambiwa miaka100 na bado angesaini sisi tungemshangaa.

Kumbe muda mwingine sio kosa lake, ila tuangalie muda na mazingira husika
Katika maisha always tunaambiwa ni muhimu kujua how much we are worth (manake kujua thamani yako) na kuhakikisha kila mmoja anajua thamani yako.

Mimi naamini Harmonize pamoja na kuwa underground na kuhangaika lazima alijua yeye ni nyota na itang'ara sana. Naamini alijiamini na ndio maana alifanikiwa sana. Kama ni mimi yeye basi ningesaini mkataba wa miaka mitano na ambao uanipatia faida pia. Ni negotiation. Unajua utamwingizia mtu hela, ni muhimu u-negotiate mkataba mzuri. Hili pia ni kwa wale wanaofanya kazi. Msiruhusu makampuni yakawaonea. Mtu fahamu thamani yako kwa mwajiri wako na omba mshahara mkubwa bila kuhofu. Sababu anajua unamwingizia hela, bado atakubali tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom