Let me tell you something! Harmonize sio Mpumbavu ingawaje anaweza kuwa mjinga!! Sio mpumbavu kwa sababu wakati yupo WCB alikuwa anafahamu thamani ya shows zake! Kwa maana hiyo, kwa kuangalia thamani ya shows zake TU bila kuangalia issues zingine kama endorsement, tayari alishafahamu idadi fulani ya shoo zake zinaweza kabisa kufidia hiyo 500M.
Lakini nimesema anaweza kuwa mjinga kwa sababu inawezekana hakutafakari kwa makini na kujua kwanini thamani/bei ya shoo zake ilikuwa hivyo! Mosi, inawezekana hakuangalia kwamba WCB ni Brand kubwa sana kwenye music industry, na kwahiyo it's obvious bei ya show za wasanii wake lazima itakuwa kubwa tu! Pili, inawezekana hakutafakari kwa makini na kujua WCB kuna negotiators wazuri wanaohakikisha Wateja wanalipa bei mzuri kwa wasanii wao!!
Ni kutokana na hilo ndo maana nikasema thamani yake wakati yupo WCB ilikuwa maradufu kuliko hiyo 500M ukichanganya na nyimbo kadhaa zilizogharamiwa na WCB. Sasa changamoto ni kwa management yake kuendelea ku-maintain na kuikuza zaidi ile status yake aliyokuwa nayo kabla hajaondoka WCB. Kama hivi sasa wanatapata basi wameshindwa ku-maintain level yake aliyokuwa nayo pale WCB. Na kwa bahati mbaya sana, hilo sio tatizo la WCB bali ni la management yake!