Je, hawa tu ndio CCM vyuo vikuu?

Je, hawa tu ndio CCM vyuo vikuu?

Mkuu Molemo,
Hivi mkate wa watoto uwa unatafuta muda gani muda wote upo JF.
 
kama kuna msomi yeyote wa chuo kikuu anayeiunga mkono ccm basi hajitambui,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,ila nadhani wamefuata hela ya kula coz boom lishaisha siku nyingi sasa watafanyaje.
 
Vyuo vikuu maana yake ni chuo zaidi ya kimoja kama hiyo ndio maana yake basi ni wachache sana.......#mtazamo.
Ndio wanachama wao kwenye vyuo vikuu hao, hakuna msomi makini wa chuo kikuu ambaye anaweza kuisupport CCM, cha kushangaza hao hao kuna siku utashangaa wanalalamika bodi ya mikopo haijawaingizia pesa yao!!
 


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokea Vijana wa Shirikisho la CCM la vijana wa CCM wlioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma.

Nape akisoma ujumbe kwenye moja ya mabango waliyofika nayo wanafuvyo hao.



Wanavyuo wakionyesha bango la kuwataka wasaidizi wa Rais kuwajibika inapobidi.

. Nape akisoma ujumbe uliloonyesha kumvutia zaidi kwenye moja ya mabango ya wanavyuo hao.

Vijana hao wakionyesha bango lenye ujumbe mahsusi kuhusu maana ya Mapinduzi.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na vijana wa Shirikisho la CCM la vijana wa CCM wlioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma

Source:Mjengwa blog
MAFISADI wa KESHO na watoto wa CCM.
Hasira za uongo tu hakuna kitu. Halafu NAPE hiyo ni Hicho kilicho sogea mbele ni ndio wanaitaga kitambi? Miye nilizoea kumuona mama yangu akiwa hivyo kwa miezi 9!!
 
Hiki ni kikundi cha kulia na kuimba misibani cha Bonyokwa. Mie nawafahamu sana.Mmoja kanipigia na kunijulisha kuwa Nape aliwakodi. Hakuna mwanachuo mwenye mwandiko mbovu kama huo.
 
Mbona kama wamachinga walikusanywa hapo kariakoo wakapewa mabango ambayo yanaonekana kuandikwa hapo ofisi ndogo ya CCM? Walikaguliwa vitambulisho vyao kuona wanasoma vyuo gani?
 
Ukipanda mahindi yana rangi gani? Kijaniii. Kudadadeki? Hayo ndo mahindi ya Lusinde naona yameota tayari.
 
hawa ndio wanaccm jasiri waliobaki ndani ya vyuo vyetu, wengine wanaionea aibu ccm yao, hawawezi kujitokeza mbele ya jamii. Na wao taratibu wataendelea kupungua
 
Maskini nimewaonea huruma kidogo nilie..Yaani hawaendani na tukio kabisa, Nape anapenda kujipa moyo
 
Inasemekana kila aliyesho up kwenye huu mwaliko wa Nape kila mtu alimegewa elf20 bajeti haikuruhusu kuchukuwa watu wengi zaidi
 
Kwa jinsi nyuso zao zilivyokata tamaa, wakirudi wote wanarudisha kadi za ccm. Wamekata tamaa, utafikiri wasipoenda wanafutiwa mikopo loan board.
 
Mkuu Molemo,
Hivi mkate wa watoto uwa unatafuta muda gani muda wote upo JF.
Nadhani hili swali ungeanza kujibu wewe mwenyewe, maana muda wote huo unaomuonaga anashinda hapa maana yake na wewe huwa unakuwa hapa.

Sasa ni vyema ungetujuza kwamba wewe unalipwa kuwepo hapa au kuharibu mijadala hapa ndio ajila yako!!...thats why unashangaa wengine kuwepo hapa? Una ufahamu wowote kuhusu Freelance?
 
Wa chadema barua zingewafata hukohuko waulize vijana wa udom waliokamatwa wakienda kwenye kampeni za Chadema kata ya chang'ombe nini kiliwakuta sema mahakama iliokoa jahazi wakarudishwa.
 
ukweli wa mambo:kwa mwanafunzi wa chuo kikuu kushabikia ccm nafsi yako lazima ikusute,maana dhambi hiyo itakutafuna mpaka uvue gamba
 
Eti kuna bango moja lina neno 'kujiuzuru' kweli mwanchuo kikuu ndiyo walivyofundishwa hivyo? Lakini ukiona mwanachuo kapewa elfu 2 anasimama na karatasi kumlaki Nape, ujue lazima yupo kwenye kundi kati ya haya

1. Walioingia vyuo kwa kufoji vyeti (akili hazifanyi kazi vizuri=mapote)
2. watoto wa wana magamba (washalishwa damu ya ccm na wazazi wao hawana njia mbadalaya kupata kipato isipokua kupitia ccm)
3. Mapepe wanaopenda kuuza sura kwenye vyombo vya hapari bila kujali hasara ya kuharibu heshima yao kwenye jamaii
4. Wenye akili za mgando -( Bendera fuata upepo) hawajitambui wanalofanya
 
Back
Top Bottom