Je haya makosa yanarekebishika?

Je haya makosa yanarekebishika?

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
Leo katika harakati za kujiandikisha vitambuisho vya utaifa Agent wao akakosea kuandika tarehe yangu ya kuzaliwa badala ya 15/01 yeye kaandika 15/10 ile ananiambia nikague info zangu ndo nikaona ilo...nikamuuliza hapa vipi akasema atarekebisha but akandelea na mtu mwingine!

Kwa wale wataalam nisaidieni je ni kweli inabadilishika? ?

Then kama tarehe ndo imekosewa ivo haitakuwa na athari?? Katika mambo yangu official ?

Asanteni!
 
Anatakiwa arekebishe kabla hajaanza kuhudumia mwingine..wewe ungekaza buti sio kuondoka
 
Anatakiwa arekebishe kabla hajaanza kuhudumia mwingine..wewe ungekaza buti sio kuondoka
Duh kwahio unaeza kuta kitambulisho kitatoka kina hio tarehe imekosewa
 
Duh kwahio unaeza kuta kitambulisho kitatoka kina hio tarehe imekosewa
Imeshakula kwako...halafu namba za kitambulisho zinakuwaga ni tarehe ya kuzaliwa ngoja baadae ntakupigia picha kitambulisho changu uone
 
Imeshakula kwako...halafu namba za kitambulisho zinakuwaga ni tarehe ya kuzaliwa ngoja baadae ntakupigia picha kitambulisho changu uone
Je Haibadilishiki mf nikienda ku request kitambulisho kipya?
 
uliangalia na mwaka mkuu? unaweza kukuta kaweka mwaka jana...stress
 
Back
Top Bottom