Je,haya yanayotokea ulimwenguni yamepangwa?

Je,haya yanayotokea ulimwenguni yamepangwa?

Habari ya wakati huu.

Wakuu mimi sio muandoshi mzuri ila kuna jambo nimeliona kule mtandao wa X kutoka kwenye akaunti fulani akizungumzia habari za matrix na mambo kadhaa ya ulimwengu kwa mifano ameonesha yote yanayotokea sasa yalishapanga yamekua programmed na system za giza zinazotawala ulimwengu.

Hapa nazungumzia yale matukio ya kuogofya ambayo sio majanga ya asili. Mtoa mada yule aliweza kuchapisha makala mbalimbali kuonesha hayo, binafsi naelewa vipo vitu vingi vya siri ulimwenguni na mambo ya giza ila sikuona ushahidi wa wazi ila huyu mdau wa X baada ya kuweka chapisho lake akataja na katuni fulani ambazo zimetabiri mambo mengi sana zinaitwa Simpson. Ikanilzimu niende kuangalia huko youtube duh ebwana kumbe kweli mambo kibaoa yalishatabiliwa kupitia katuni hizi miaka kadhaa iliyopita ikiwemo ishu ya Donald Trump kurudi tena madarakani na kunisurika kifo.

Hapa naona kabisa kuna mambo yanachezwa na watu wenye ulimwengu huu kwasababu hakuna utabiri wa namna hii wa picha kabisa tena unahusu jambo fulani na kweli yanatokea miaka kadhaa mbele kumbe Kuna wahuni wanaendesha hii dunia hao ndo wanaamua iendaje.

Hapa nimeweka baadhi ya screenshot na video ya katuni hizo. Unaweza kwenda Youtube pia ukajionee hizi katuni za Simpsons.
- Season epsode ya 11 ya mwaka 2000 (Bart to the Future) ilitabiri Donald Trump atakuwa president.
  • Season episode ya 23 ya mwaka 2012 (Lisa Goes Gaga) ilimuonyesha lady Gaga akiwa amevaa mavazi fulani akitumbuiza, mwaka 2017 kwenye super bowl alivaa mavazi yale yale na kufanya matendo yale yale.
  • mwaka 2010 walisema Bengt R Holmstrom atashinda Nobel Prize ikatokea kweli miaka 6 baadae akiwa na Oliver Hart
Kitabu kinaitwa end of time prophecy kiliongelea kuja kwa corona virus na ikawa kweli.
 
Vipi hadi vitabu kabisa , nitakuwa na uppload humu kimoja baada ya kingine
Maana si rahisi kuvipata kwenye websites hizi za kawaida za vitabu ,mpaka uzame deep web (dark web)
Baadhi ni hivi
Yaani ukiwa unapitia hizi cartoons tuliza akili kuna vitu vingi utagundua
Hawa washenzi wameweka ujumbe mzito sana kwenye hizi series
Shukrani nitavipitia
 
Hivi nikwamba leo ndio umejua hilo?? Kua dunia ni matrix.
Mbona hua nafundisha sana kuhusu hilo.
Kwa taarifa kamili nikwamba upo kwenye matrix100%
ila huwezi nielewa.
Usichanganye vitu man,mimi najua sana kuna mambo ya siri yanaendelea ila sikuwahi kuwaza kua kuna katuni imefunua mambo mengi kwa maigizo tena ikitumia image zile zile za wahusika.
 
Kuna hichi kitabu cha the secret terrorist hii kitu ukisoma unaweza kuzimia namna dunia inavyo endeshwa kwa uongo mfano vita ni mipango ya watu flani ili kutimiza mipango yao tukio kama la 9/11, kuzama kwa meli ya titanic nk . Mwandishi kagusa hadi dini mfano kwanini ukristo umekuwa na madhebu mengi pia kagusia dini ya Uislam kwamba ilianzishwa ili ilete usawa na pia itumike pale ambapo vatcan itashindwa kupenya. Tunaishi kwenye ulimwengu hatari tupu.
 
Back
Top Bottom