- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliendelea na Operesheni ya Katiba Mpya kwa Kanda ya Victoria tarehe 17 Mei 2026 Geita Mjini, ikiongozwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho John Heche akiambatana na viongozi wengine.
Madai
Kumekuwapo na taarifa iliyochapishwa na ukurasa wa simpleetz katika mtandao wa X na Facebook ukieleza kuwa akiwa Geita mjini John Heche alisema Watanzania wafahamu kuwa CHADEMA hawajakataa maridhiano kama wengine wanavyosema.
"Lazima Watanzania wafahamu kuwa sisi CHADEMA hatujakataa maridhiano kama wengine wanavyosema na ushahidi ni huu hapa tunafanya mkutano yetu kwa amani bila tatizo lolote, wapuuzeni hao kuwa CHADEMA wamekataa hapana ila sisi ndo tume taka Maridhiano"
Je, ni kweli kauli hiyo imetolewa na Heche?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kupitia marejeo ya video ya mkutano wa CHADEMA Geita mjini umebaini kuwa nukuu hiyo si ya kweli kwani Heche hakutoa kabisa kauli hiyo.
Nukuu hiyo inapotosha uhalisia wa kilichozungumzwa na kiongozi huyo ambaye akizungumza kwenye mkutano huo.