Je, hii imekaaje?

Je, hii imekaaje?

mj909

Member
Joined
Aug 1, 2024
Posts
86
Reaction score
204
Kama kuna Mtaalam wa Afya anisaidie hivi kwamfano mtu akipima na akakuta anamimba halafu baada ya siku ya hedhi akatokwa na damu kwa siku moja tu kisha akaenda hospital kuangalia.

Akaambiwa ujauzito umetoka japo akipima kipimo cha mkojo kinaonyesha ana mimba ila ultrasound inasema mimba imetoka kumbuka hapo nimimba ya Wiki Mbili tu.

Halafu baada ya Wiki moja kupita akaanza kuhisi dalili za mimba wakati hapo awali hakua nazo.

Sasa inanichanganya itakua imetoka kweli au itakua bado ipo?
 
Homoni za mimba zinaendelea kujionyesha kwenye upt hata baada ya ujauzito kuharibika kwa ushauri zaidi muone daktari.
 
Haipo...kipimo huwa kinasoma tu...week mbili zingine zikikata hakitasoma positive tena
 
Ukimchinja kuku na apo apo ukamwachia kuku bado ataendelea kujongea na baada ya muda atakufa tu...huu ni mfano tu
 
Homoni za mimba zinaendelea kujionyesha kwenye upt hata baada ya ujauzito kuharibika kwa ushauri zaidi muone daktari.
Unazungumzia kwamba zinaendelea kwenye kipimo... Je na dalili anazoziona?
 
Back
Top Bottom