Je, hii inaweza kuwa anxiety disorder?

Je, hii inaweza kuwa anxiety disorder?

Joined
Sep 10, 2019
Posts
17
Reaction score
15
Kipindi nasoma advance mzazi wangu alinionya na kuniambia jirani yangu ana mamb ya kichawi ,na nilikuwa sipendi kabisa wajue mambi yangu hususan ninasoma wapi.

Ikatokea siku nikiwa nalipa ada kwa wakala baada ya kumaliza wakati naondoka nikamuona mtoto mmoja wa ile familia akiwa mazingira yale, hii ikaniogopesha sana na kuhisi labda atakuwa kaona shule ninayosoma na pengine kunifanyia Jambo baya.

Hii ilinisumbua sana nikashindwa kufanya mmb yangu ,Kama kujisomea, nikakosa raha kweli kweli ,nikawa depressed, masomo yangu yakaenda vibaya ,ndani kipindi kirefu Kama miezi 4 hivi Hadi pale tulipofanya mitihani ya mwisho.

Nilipoona nimefanya na kumaliza, yale mawazo yakaondoka na nikawa na amani .Sasa ninajiuliza hii Ni nini na jee unahusiana na anxiety disorder labda?
 
Back
Top Bottom