Je, hii 'Media Blackout' ya leo juu ya tukio zima la uchukuaji fomu wa Tundu Lissu ndiko kumuenzi vyema Mwanahabari Hayati Rais Mkapa?

Mkuu sijamaliza vyote ulivyoandika. Maana hata madai yenyewe kumbe huna uthibitisho nayo! Bora ungekaa kimya.
 
Kweli vichaa mko wengi sana.

Tar 15 tukutane taifa ili kuona maandalizi ya kampeni kupitia wasanii 109 watakaosambaa nchi nzima kuanzia tar 27 agositi.
Mnategemea wasanii badala ya Sera???? Kweli CCM mmepoteana mwaka huu
 

Gentamycine kwanza nikupongeze kwa kuwa mmoja wanaccm wachache sana, ambao mmekuwa na uthubutu wa kuongea ukweli ulio kinyume na wanaccm wengi. Kwa hili nakuheshimu.

Ni kwanini tumefika hapa? Siku zote huwa tunalalamika kuwa katiba ya nchi yetu imepitwa na wakati, na madaraka ya ofisi namba moja yamevuka mipaka, kiasi kwamba tabia binafsi za namba moja, zina uwezo kabisa wa kugeuka ndio tabia za uendeshaji wa nchi. Namba moja kama namba moja ni mchapakazi kwa asili, bila kujali uchapa kazi wake una faida kiasi gani, na hasara kiasi gani. Ila namba moja hayupo kwenye siasa kwa uwezo japo anaipenda siasa, lakini siasa haimpendi.

Inaonekana namba moja anashindana na wakati, sio kwamba ccm haijafanya kitu nchi hii, au yeye hajafanya kitu, ila kwa nature ya binadamu huwa ana tabia ya kuchoka kitu. Kwa sasa watu wameichoka ccm, ndio maana inakaa madarakani kwa mabavu zaidi kuliko ushawishi. Na hao wanaotaka kuingia sio kwamba ni lazima wawe wazuri kuliko namba moja, au watafanya vizuri kuliko ccm, hapana, ila hiki ni kizazi chao. Sasa wanaccm wachache kama nyie msiposimama na kusema tuache nature ichukue nafasi yake, huenda nchi ikaingia kwenye machafuko, au isipoingia kwenye machafuko kwa ajili ya hofu ya wananchi, kutakuwa na chuki, na mgawanyiko. Na serikali itaongoza kwa kutumia mabavu na sheria nyingi kandamizi. Sababu hasa ni kulazimsha kuongoza against nature.

Kwasababu ya kulazimisha kuongoza kizazi tofauti, tutajionea uchaguzi mwingine wa kishenzi kama ule wa SM. As a result, itabidi kiongozi huyu aendelee kukaa madarakani zaidi ya miaka 10, au amuachie kiongozi mwingine roho mbaya, ambaye atakuwa analazimisha kupendwa kama yeye. Vinginevyo akiingia kiongozi mwingine mwanadiplomasia atapelekea ccm kutoka madarakani kwa aibu kutokana na balance of nature. Mwanamke hata akiwa mrembo vipi, akishazeeka kazeeka tu, ili aendelee kuvutia wanaume itabidi atumie nguvu kubwa kama hela, ushirikina nk. Lakini hata wanaume atakaowapata sio kwakuwa wanampenda, bali watakuwa wanafuata hela na nguvu zake za ushirikina. Hii ccm yako kwa sasa naifananisha na mtu anayelazimisha kuvuta riziki kwa kamba. Huyo Lisu anapendwa tu, hata kama hana lolote la maana analoweza kufanya. Hivyo mwambieni namba moja kuwa wakati ukuta.
 
Ninaanza kuamini taratibu kuwa yawezekana kuna 'Wanafiki' na 'Wapumbavu' fulani 'wanamshauri' vibaya na 'Kumponza' Kisiasa Rais wangu JPM.
Wapo! na wanafanya hivyo ili kupambana na njaa za matumbo yao si maslahi mapana ya taifa na ustawi wa ccm kama chama tawala. Watamponza na wataliponza taifa.
 
Nimestaajabu ya Mussa nikakuona Firauni, Toka lini ulikua mwana CCM bana.

KTN, BBC, DW, SBC wataripoti hakuna shida "usitufikee"
 
GENTAMYCINE wewe nakuaminia upo very OBJECTIVE kwenye issue za msingi na Uchama unaweka kando.

Hongera sana kwa uchambuzi MUJARABU. Nisamehe some time nakuchukiaga 👊👊👊
 
Kuwa na akili hata kidogo basi. Unafikiri nani ataiamini chadema media bila kuhakiki habari kwenye chombo huru?
Halafu unajitoa akili kama chadema hawakuwa na Tanzania Daima ambalo limefungiwa. Je wasingefungia hicho ukisemacho? Kwanza TV online media huru imefungiwa. Kwa uwastani vyombo vilivyobaki vyote haipo huru
 
Umesema hujathibitisha hizi tuhuma za waandishi kuzuiwa kuripoti habari ya Lissu, sasa inakuaje unalaumu jambo ambalo huna uhakika nalo.

Mpaka sasa kuna wagombea wangapi wamechukua fomu na siyo vyombo vyote vya habari vimeripoti, why ulalamike kwa Lissu peke yake au wengine siyo wagombea?

Kumbuka vyombo vingi vya habari hasa nyakati hizi za uchaguzi vinafanya biashara. Hakuna Mkutano wa chama cha siasa au shughuli yoyote ya chama cha siasa isiyolipiwa. CCM wanalipia coverage zote mikutano yake ya kisiasa kuanzia magazeti mpaka televisheni. Isitoshe wana TV yao (Channel 10) radio (uhuru fm) na gazeti lao (uhuru). Yote haya yanarusha shughuli zote za chama chao.

CHADEMA waliposhauriwa kuwekeza kwenye media waliwaona watu wajinga matokeo yake ruzuku yao inaishia kwenye matumbo ya wachache. Sasa hivi wanalialia wanataka kufanyiwa hisani. Hakuna hisani wala huruma, Media zote zinafanya biashara. Huna fedha usitegemee habari yako itaripotiwa popote au kupewa coverage ya kutosha. Mpaka Mkutano wao wa kuchagua mgombea u Rais wameshindwa kuulipia ukapata coverage ya kutosha.

Mwaka 2015, Lowassa alitumia fedha nyingi kwenye kampeni ikiwemo kupata coverage kwenye TV na magazeti kwa shughuli zake zote za kisiasa. Sasa kama Lissu hana fedha wala CHADEMA haiwezi kumsupport mgombea wake, kwanini mnataka kuibebesha mzigo CCM na Serikali yake eti wanatoa maelekezo kwa media zisirushe matukio ya Lissu. Hizi ni akili za kitoto na propaganda za kipumbavu.

Kama hizi tuhuma ni za kweli, basi watuambie ni chombo gani cha habari ambacho walitaka kulipia kirushe shughuli zao za kisiasa halafu kwa sababu yoyote ile chombo hicho kikakataa kufanya hivyo.
 
Kweli vichaa mko wengi sana.

Tar 15 tukutane taifa ili kuona maandalizi ya kampeni kupitia wasanii 109 watakaosambaa nchi nzima kuanzia tar 27 agositi.
Kumbe mnategemea wasanii wawajazie uwanja?

Huko Zanzibar hasa pemba ukiona ccm ina idadi kubwa ya watu ujue imebeba watu kutoka bara na unguja na wasanii ili vijana wavutiwe kwayo lakini kinyume chake hawawezi na hawathubutu maana aibu ya kutokuwa na watu watajicheka wenyewe.
 
Halafu wala haifiki $ 10,000 /=

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakinunua hivyo nawafungia bure kabisa, na kadi ya black magic nawapa

Nashindwa kuamini CDM ktk media wanafeli vipi ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Media house watakula wanakopeleka mboga post election
 
Spika ya Mabeberu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…