Uchaguzi 2020 Je, hii ndiyo sababu ya NEC kutochapisha fomu za wagombea Urais kwa "Alphabetical order"?

Jambo la msingi ni kujua shetani alitawala na ataendelea kutawala upende usipende hata kama wanadamu hawampendi
 


NEC NA ZEC TOENI UFAFANUZI.

JE, KIPEPERUSHI KINACHOTUMIWA NA CCM KIMETOLEWA NA TUME?

JE, KINA BARAKA ZA TUME?

JE, NI HALALI?

JE, MAADILI YA UCHAGUZI YAMEFUATWA?
 
Wamekosea sana kumuweka JPM pamoja na hawa wasio hata na chembe ya uzalendo. Wamekosea sana
Kwanini uone wamekosea? Ulitaka kila mgombea wa Urais awepo kwenye karatasi yake?

Kwa taarifa hao wagombea ni wazalendo ndio maana vyama vyao vimewaamini na kuwapa ridhaa ya kugombea.
 
Kwa maana hiyo wakiona unavuta karatasi na kushuka chini, roho zinawaenda mbio, wanajua unamtafuta Lissu...



Cc: mahondaw
 
Mwamba ngoma huvutia kwake,

Sasa hapo ingeonekana HAKI kama Chadema ndio ingeoenekana katika nafasi ya CCM.
 
Sijasikia TL akitoa elimu hii. Kwa kweli kwa hili CHADEMA wamelala.
 
Huko Huko mwisho ni vizuri wamerahisisha kutafuta kuliko ingukuwa ktkt unasema tu weka tick chini mwisho
Chadema ingewekwa karibu na Chauma watu wangebabaika lkn kule mwisho mbona ni raha tupu wala mtu aangaiki kutafuta
 
Haya ndio matatizo ya kutokuwa na Tume Huru..ukiambiwa unafuata tu ..ila hii bado haijabadilisha kitu Lissu atashinda kwenye sanduka la kura
 
Hivi kwa nini CCM mnapenda kuwaona Watanzania wote hawana akili isipokuwa nyie peke yenu? Watanzania wa sasa ambao asilimia kubwa ya wapiga kura wana miaka chini ya 40 na Elimu ya kuanzia kidato cha NNE shule za kata hata kama walipata dv4 ya mwisho washindwe kusoma na kuweka tick wanapopataka!!? Acheni kudharau wananchi kiasi hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…