Habari zenu ndugu wana JF, leo usiku niliona maono au niliota ndoto mtu mwenye silaha ya kivita (SMG, AK47) akimnyooshea hayati Magufuli kana kwamba anataka kulipa kisasi na watu wanaoshuhudia wakiwa hawana la kufanya. Baadaye ilionekana kama hayati alifanikiwa kukimbia na yule mtu kumkimbiza akiwa kamnyooshea silaha na palepale nikaamka. Je, kuna uwezekano hii ni roho ya kisasi?
Ukisoma maandiko kitabu cha Mwanzo 4: 1-14 kuna habari ya Kaini kumuua ndugu yake Habili na Mungu kumhoji kwenye mstari wa 10 'Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi'. Hii maana yake ni kwamba damu ya mtu aliyeuawa ina tabia ya kudai kisasi kwa yule/wale waliohusika na kuimwaga. Hii ni tofauti na damu ya Yesu Kristo kwa tunaosoma biblia, yenyewe inanena mema, inatoa au inasukuma roho ya msamaha hasa ukirejea alipokuwa pale msalabani pamoja na mateso yote yale bado aliweza kuachilia msamaha kwa watesi wake 'baba wasamehe hawajui walitendalo'.
Haya maono yanaleta ujumbe kwetu ambao bado tupo hai tuungane katika maombi ya msamaha na rehema kwa Mungu kumwombea ndugu yetu hayati Magufuli na kwa walio na kinyongo dhidi yake waachilie roho ya msamaha. Kwa sababu haya maono yanahusisha kiongozi wa ngazi ya juu kabisa hili pia linapeleka ujumbe kwa watawala kujitahidi kutenda haki na kujiepusha kumwaga au kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye maangamizi ya watu wasio na hatia. Katika hili kipekee kabisa tumwombee rais wetu ajitahidi kuwa na moyo wa unyenyekevu wa kutenda haki kwa watu wote na kukemea kwa nguvu zote matukio ya watu wasio na hatia kupoteza uhai katika mazingira yasiyoeleweka.
Nawasilisha.