Je, hii ndoto/maono juu ya hayati Magufuli inatuhitaji tumfanyie maombi ya msamaha na je, inapeleka ujumbe kwa watawala?

Nyumisi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
13,499
Reaction score
19,292
Habari zenu ndugu wana JF, leo usiku niliona maono au niliota ndoto mtu mwenye silaha ya kivita (SMG, AK47) akimnyooshea hayati Magufuli kana kwamba anataka kulipa kisasi na watu wanaoshuhudia wakiwa hawana la kufanya. Baadaye ilionekana kama hayati alifanikiwa kukimbia na yule mtu kumkimbiza akiwa kamnyooshea silaha na palepale nikaamka. Je, kuna uwezekano hii ni roho ya kisasi?

Ukisoma maandiko kitabu cha Mwanzo 4: 1-14 kuna habari ya Kaini kumuua ndugu yake Habili na Mungu kumhoji kwenye mstari wa 10 'Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi'. Hii maana yake ni kwamba damu ya mtu aliyeuawa ina tabia ya kudai kisasi kwa yule/wale waliohusika na kuimwaga. Hii ni tofauti na damu ya Yesu Kristo kwa tunaosoma biblia, yenyewe inanena mema, inatoa au inasukuma roho ya msamaha hasa ukirejea alipokuwa pale msalabani pamoja na mateso yote yale bado aliweza kuachilia msamaha kwa watesi wake 'baba wasamehe hawajui walitendalo'.

Haya maono yanaleta ujumbe kwetu ambao bado tupo hai tuungane katika maombi ya msamaha na rehema kwa Mungu kumwombea ndugu yetu hayati Magufuli na kwa walio na kinyongo dhidi yake waachilie roho ya msamaha. Kwa sababu haya maono yanahusisha kiongozi wa ngazi ya juu kabisa hili pia linapeleka ujumbe kwa watawala kujitahidi kutenda haki na kujiepusha kumwaga au kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye maangamizi ya watu wasio na hatia. Katika hili kipekee kabisa tumwombee rais wetu ajitahidi kuwa na moyo wa unyenyekevu wa kutenda haki kwa watu wote na kukemea kwa nguvu zote matukio ya watu wasio na hatia kupoteza uhai katika mazingira yasiyoeleweka.
Nawasilisha.​
 
Bro Mungu anajitambulisha mwenyewe kuwa Yeye ni Mungu wa walio hai si wafu

Sasa Mzee kapumzika mwacheni pambaneni na khali zenu
 
Wenye vinyongo wasamehe?! Yaani mtu alifanyiwa unyama kwa amri ya mkulu halafu aseme amesamehe kwa kuwa tu umeota SMG ya Hamzaboy...huku bado anaigulia maumivu makali kutokana na unyama wa bwana yule
 
Wenye vinyongo wasamehe?! Yaani mtu alifanyiwa unyama kwa amri ya mkulu halafu aseme amesamehe kwa kuwa tu umeota SMG ya Hamzaboy...huku bado anaigulia maumivu makali kutokana na unyama wa bwana yule
Mkuu pamoja na Yesu kutokuwa na hatia yoyote bado alitoa msamaha kwa watesi wake, wewe mwenzangu na mimi uliyejaa dhambi na uovu, unapokataa kuachilia msamaha unategemea nini kutoka kwa Mungu uliyemtendea dhambi na binadamu wenzio uliowahi kuwakosea......tafakari.
 
Mwombee wewe uliyeota.Ndoto zako hazituhusu.
Kama mlitumana huko kudhulumu mtu haki yake kuishi hukumu i kweni
 
Washauri pia waliyopo,
Wanaoendelea kujivunia ukatili na kushabikia udhalimu wa Mwendazake waende wakaongozwe kwenye sala ya TOBA.
Waachane kabisa na mambo ya shetani ya kutesa, kubumba na kubambikia watu mikesi.
AMEN
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…