Je hii ni Hali gani ya kutopenda kula na kunywa vitu vitamu

Cute Msangi

Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
79
Reaction score
226
Tokea nikiwa mdogo nilikuwa sio mpenzi wa kula na kunywa vitu hivi na mpaka nimekuwa nimekuwa na allergies navyo havinidhuru Ila sipendi kula

*Maziwa ya ng'ombe

*Mayai
*Nyama ya kuku,mbuzi,ngombe nakula kidogo Sana napenda utumbo
*Chapati
*Chakula chochote au mboga yeyote yenye mchuzi,mfano lost ya nyama nk
*Tambi
*Chipsi
*Soda na juice za madukani
*Keki
*Sambusa napenda Nile viazi au viungo vya ndani
Maandazi nakula tu Ile ngozi ya nje iliyoiva Basi watu wananishangaaga Sana.
*Vitunguu maji vilivyoiva vikiwa kwenye mboga nikioviona tu hamu ya kula inaisha.
*Samaki
*Dagaa

Nimekuwa napata tabu Sana nikiwa ugenini kula vyakula vyao muda mwingine najilazimisha tu siunajua ugenini uwezi kuforce unachotaka.

Je hii ni Hali ya kawaida kutopenda kula na kunywa vitu vitamu.
 
Akili yako toka utotoni umeiaminisha kua hivyo vitu huvipendi,ni issue ya mind mentality tu,issue ya kisaikolojia,badili fikra zako kwanza kisha utakula tu hivyo vitu coz umesema havikudhuru.
Kweli Mkuu hata mimi nilijitengenezea sinywi mtindi tokea nikiwa mdogo ila nilikuja kuivunja baada ya maisha ya ghetto na kibachela kunichapa hvy ikawa mboga ya bei rahisi na ya Chap( Huku kwetu tunaita suti[emoji23][emoji23]).....

Mfano mpaka sa hivi nakunywa pombe ila mbege sionji kabisaaaaa........., Mpaka watu huwa wananishangaa mimi mchaga wa aina gani
 
Pole sana ila tatizo lipo sehemu vyakula vyote hivo huli sasa unapata mlo kamili kweli?
 
Maandazi unakula ngozi ya juu iliyoiva ila sambusa ngozi ya juu iliyoiva hapana,, duuh pole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…