Drat
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 1,160
- 1,359
Habari zenu?
Natumaini wote mko salama.
Je, hii ni njia mpya ya kutengeneza kipato? Is this a new hustle? Mara kadhaa imewahi kunitokea katika simu nakuta hela inakatwa, kama vile nimeongeza vocha halafu nataka kuunga kifurushi naambiwa salio halitoshi.
Kipindi cha nyuma nilikuwa nasamehe kwa kudhani labda kwa kuwa ni huduma ambazo unaambiwa "bonyeza nyota au kitufe chochote kupata huduma hii" basi huenda niligusa kwa bahati mbaya.
Lakini hii ya juzi juzi imenifikirisha sana, nikawaza niwaulize wakuu inawezekana hii ni hustle mpya, tena ya kikatili.
Pesa ilipokatwa nikapiga simu kwa mtoa huduma wa kwanza, yeye akasema nimejiunga huduma fulani na hayo ni makato,nikamthibitishia sijajiunga na nina uhakika asilimia zote hakuna mtu anagusa simu yangu, na mimi sijafanya jambo hilo. Basi akanielekeza namna ya kusitisha huduma,nikasitisha. Hakutaka kutoa maelezo akakata simu.
Baada ya kujitoa, nikaamua kucheki hatua za kujiunga na huduma hiyo, nikakuta njia ni kuandika ujumbe fulani nakutuma kwenda katika namba fulani mfano wa 155**, kwa hatua zile nikajua kuwa hawa watu walikata pesa.
Nikaamua kupiga tena nipewe ufafanuzi, kwa kifupi nilijibiwa, umeshafanikiwa kujitoa suala hilo halitatokea teana,nilipouliza kuhusu hela yangu kurudi, jamaa akatema script ya kuagia kisha akakata simu.
JE NI NJIA YA KUTENGENEZA KIPATO?
Wakali wa mifumo ya kimtandao naomba mnijibu,je inawezekana third party company ya kutoa huduma kama hizo za hadithi, sijui stori za kurwa na doto wa kariakoo kufanya namna pesa ikakatwa bila ridhaa? Na je serikali kupitia vyombo vyake wanafatilia ili kutulinda?
Wanasheria je kupitia baraza la ushindani mtu anaweza kudai pesa yake irudishwe hata kama ni ndogo?
Niliwaza kwa siku ile na kwa kusamehe kule kama ilifanyika kwa watu milioni moja, jamaa waliingiza 100,000,000 kwa muda wa chini ya lisaa.
Kama ni hustle, basi na sisi tukajipange nayo. Nchi bado mbichi, unapigwa kisha unakaa kimya imetoka