Je, hii ramani imekamilika?

Je, hii ramani imekamilika?

Saad30

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2020
Posts
2,737
Reaction score
5,464
Habari nyingi wakuu..

Katika ujenzi ambao nataka nianze Inshaallah baada ya kumaliza mambo mengine sasa nimechorowe ramani hii hapa kutokana na nyumba yangu nataka iwe hivi.

Hivyo basi wakuu humu kuna magwiji wa haya mambo ya ramani pamoja na ujenzi wake.Naomba kufahamu kutoka kwenu je hii ramani ipo sawa ama la.

Vipi hadi kuisha kwake gharama zake Shilingi ngapi?

Ramani.JPG

Nawasilisha.
 
Attachments

Ramani iko poa tu kuhusu gharama ngoja wajuzi waje ila aliyechora mara nyingi anaweza kutoa makaidirio lakini njia rahisi mtafute fundi
 
3 bedroom house,
Boma na kuezela on average ni 22-27 M,
Finishing ya kuingia ndani mi 13, finishing ya ukweli kabisa ni 25M,
In total uwe na 50M ili nyumba iwe classic, Ila kama ni kuhamia Tu then finishing nyingine umalize ukiwa ndani basi Anza na 35M
 
Pesa ya kuanzisha kampuni kabisa hii 50M

Ila wacha tuone kikubwa kuwa na raha kwenye banda lako hata ukinywa uji waswahili husema hivyo
 
3 bedroom house,
Boma na kuezela on average ni 22-27 M,
Finishing ya kuingia ndani mi 13, finishing ya ukweli kabisa ni 25M,
In total uwe na 50M ili nyumba iwe classic, Ila kama ni kuhamia Tu then finishing nyingine umalize ukiwa ndani basi Anza na 35M
Uwongo
 
Ramani nzuri lakini mimi ningekuwa mchoraji ningefanya mabadiliko matatu.

1. Front porch (baraza la mbele) ningeiweka hilo eneo kati ya dining na living room, hii ingesaidia kusave nafasi kwa mahali ambapo hilo baraza lipo sasa kuondoka

2. Ningefanya vertical flip ya masterroom, yaani kulipo mashariki kuwe magharibi na kinyume chake, nia ya kufanya hivi ni ili nifanye sebule iwe wazi zaidi kwa kuangusha huo ukuta unaotenga sebule na korodo ili uwe wazi (open floor concept).

3. Ningetoa huo mlango wa sasa kutoka sebule kwenda vyumbani.
 
Choo cha master kidogo sana. Nashauri ile passage ya master ingenyooka kwenda jikoni na mlango wa master ungewekwa karibu na bedroom ya kati. Hilo litawezesha kupata nafasi kubwa ya choo na wardrobe ya master

Pia choo cha Public hakuna haja ya kuweka kuta kuta kati ya choo na bafu. Ingekuwa toilet kubwa yenye bafu na sink ndani. Pia ungepata nafasi ya kuweka facilities nyingi za kisasa. Mtindo uliotumika ni wa mwaka 47

Anyway nyumba ya kawaida ambayo ukipata hela utaiona kituko na kujenga nzuri zaidi hiyo uifanye hostel ya watoto wa chuo
 
1. Hakuna ulazima wa kuweka mlango kati ya dining na kitchen
2. Mlango wa Public toilet ingekua mwanzoni hapo ingekua poa zaidi.
3. Very long corridor ni wastage of space.
4. Ingekuwepo opening kati ya corridor na sitting room ingependeza
5. Mlango wa kitchen na lounge ifungukie nje.
................ Etc
 
Ramani nzuri lakini mimi ningekuwa mchoraji ningefanya mabadiliko matatu.

1. Front porch (baraza la mbele) ningeiweka hilo eneo kati ya dining na living room, hii ingesaidia kusave nafasi kwa mahali ambapo hilo baraza lipo sasa kuondoka

2. Ningefanya vertical flip ya masterroom, yaani kulipo mashariki kuwe magharibi na kinyume chake, nia ya kufanya hivi ni ili nifanye sebule iwe wazi zaidi kwa kuangusha huo ukuta unaotenga sebule na korodo ili uwe wazi (open floor concept).

3. Ningetoa huo mlango wa sasa kutoka sebule kwenda vyumbani.
3. Huo ukuta nadhani umeachwa mahsusi kwaajili ya decoration ya TV wall.
 
1. Unakuta mahitaji yake anataka sebule iwe na madirisha mengi ili hewa ipite kwa wingi. Akiweka baraza hapo kati inapoteza mwonekano na itafanya madirisha yawe madogo au yasiwepo kabisa.
Vilevile kwa kuweka baraza iliyo extend mbele namna hyo inasaidia kupaua kwa kuweka "gebo" ambapo inaleta mwonekano mzuri zaidi.
 
TV wall itahamia huu upande mwingine wa kushoto ambao sasa una mlango wa kwenda vyumbani...
 
1. Unakuta mahitaji yake anataka sebule iwe na madirisha mengi ili hewa ipite kwa wingi. Akiweka baraza hapo kati inapoteza mwonekano na itafanya madirisha yawe madogo au yasiwepo kabisa.
Vilevile kwa kuweka baraza iliyo extend mbele namna hyo inasaidia kupaua kwa kuweka "gebo" ambapo inaleta mwonekano mzuri zaidi.

Mkuu, hata baraza likihamia hapo nimetaja halitazuia uwepo wa madirisha mengi na sijajua hiyo theory ya kwamba baraza hupunguza ukubwa dirisha umeitoa wapi?

Kuna uwezekano baraza likawa la 'gebo' au slab, hatuna uhakika kwa sababu ramani haijaonesha mchoro wa bati
 
Back
Top Bottom