Mizania
JF-Expert Member
- May 17, 2023
- 3,812
- 3,277
Mkuu tujikite kwenye wimbo huu wa 'Nitasema', ni maneno gani ndani ya wimbo huu ambayo ni ya hovyo na yanayokera???Wasanii kibao wameimba nyimbo za kiharakati na kukosoa ila hawajawahi kukamatwa. Mr II, Wagosi wa kaya, Prof Jay na Joh Makini wana nyimbo za kuhoji mambo ya kitaifa lakini hawajawahi kubugudhiwa. Wao hawatumii maneno ya kukera kufikisha ujumbe. Nay wa mitego kwa upumbavu wake hutumia maneno ya hovyo yasiyovumilika ndo maana anasumbuliwa. Wagosi waligusa kila sekta lakini fresh tu walieleweka. Joh Makini baada ya vurugu za Arusha mwaka 2011 alitoa wimbo wa Bye Bye lakini naye hakufanywa kitu. Nay ajifunze kwa waliomtangulia.
Hebu tuainishie hayo maneno hapa nasi tuyaepuke!! Yanakera kivipi?? Maana hata Basata kwenye hukumu yao hawaja sema yanakera au ni ya hovyo, wamesema wao wameona hayana ushahidi!!
Mkuu wewe hii hukumu yako ya kwamba maneno hayo ni ya hovyo na yanakera umeitoa wapi?? Kwa kanuni na sheria ipi tofauti na ya Basata???