Je, hili limekukuta kuachwa na bus kisha ukatumia bodaboda kulifukuza bus

Je, hili limekukuta kuachwa na bus kisha ukatumia bodaboda kulifukuza bus

Ukiambiwa ufike stand saa 11, ukagika saa 11 kasoro na basi halipo usihangaike kulifukuza waambie tu wameyatimba maana umewahi na wao wameleta usela. Kuna Mabasi wanakwambia fika stand saa 9, saa 9 na nusu tunaondoka. Ukifika saa 8 na dakika 50 unaambiwa washasepa wakimbize.
Nasikia dawa yao ni LATRA tu
 
Mimi ilinitokea mwaka juzi tunaenda msibani nmekata siti za kutosha 480000, fresta ikatuacha. Shida tulikuwa na watoro so kuifukuza na boda tusingeweza. Fresta nyingine ikatubeba tukaja ikuta moro, konda wa fresta iliyotuacha alimaindi nadhan alikuwa ashaona atauza siti
alishazipigia hesabu hizo siti hapo moro angebeba abiria wake
 
Niliachwa na gari msamvu , nyehunge ya kuelekea mwanza .
Nilipatwa na msiba wa mke nikapewa ruhusa ya kupumzika nikaamua kurudi nililozaliwa kupumzika .Stress zilinifanya niamke saa 6 siku inayofuata badala ya saa 11 .Tokea hapo hua sikati tiketi tena hata iweje yaani
 
Niliachwa na gari msamvu , nyehunge ya kuelekea mwanza .
Nilipatwa na msiba wa mke nikapewa ruhusa ya kupumzika nikaamua kurudi nililozaliwa kupumzika .Stress zilinifanya niamke saa 6 siku inayofuata badala ya saa 11 .Tokea hapo hua sikati tiketi tena hata iweje yaani
pole sana mkuu
 
asante.
ila safari nyengine kama itatokea hivi sisumbuki kuwakimbiza ni kuipigia mamlaka alafu watanyooka
Kuwakimbiza na ile speed hapana aiseee ni bora usubiri kesho au upande gari lingine maana wanakuwaga na muda wa kutoka tofauti tofauti kwa hiyo hiyo kampuni
 
Mimi nimeexperience kinyume

Nishawahi kukata tiketi gari la kuelekea Dodoma (nadhani ilikuwa alsaedy au super champion)
Nimekata tiketi saa 2 na walisema litaondoka saa 2 ½, kibaya naingia ndani nakuta abiria kama watano tu nikasema leo nimeyakanyaga

Nimejaribu kwenda Kwa konda akawa anakazia abiria wapo wengi tu wametoka nje na akanionyesha kitab Chao Cha tiketi kweli kilikuwa kinakaribia kujaa


Tukikaa kwenye gari kuanzia saa 2 hadi saa 5, kibaya zaidi gari lilikuwa lipo limewashwa likazimwa na wakalipaki pembeni kabisa kuonesha hakuna ratiba ya kuondoka

Kuna jamaa mmoja, akawafuata makonda akawaka sana na akawaambia wamrudishie nauli yake huku wengine tupo kimya tu tunasapoti kimoyomoyo


Jamaa wakataka kumrudishia Hela yake akagoma akasema yeye atakuwa wa mwisho kupewa, yaani Hela Kila mtu apewe nauli yake ili akapande gari lingine

Jamaa wakapagawa wakaamua kuanza safari.


NILICHOJIFUNZA
1. Hutakiwi kuwasikiliza maagent vishoka maana waliniongopea gari kama kimbinyiko, shabiby nk zimejaa kumbe uongo

2. Sikuwahi kukata tiketi mpaka niingie ndani ya gari nijirishishe kuwa lina abiria wa kutosha

3. Kusafiri na kampuni za uhakika sio magari mabovumabovu /ya zamani
Mm walishawahi niingiza choo cha kike,tena mwanamke basi sitaki kuwasikia had leo
 
Niko naelekea kigoma kabla ya stand ya chalinze km kama 5 hiv kuna vx iligongana na lori la mchanga sasa ikasababisha foleni
Nikashuka ku****a bwana nakuja kurud bus ishaondoka aiseee boda chap mpaka stand ya chalinze naikuta bus ndo inatoka boda anataka 5000 na mm nina 10 hana chench nilihahaaa aisee jirani yangu ndo akaniazima 5000
Betrice popote ulipo kunywa peps kwa mara nyingne ulinisave sana siku hiyo
Hii hatua unaweza kumsusia chenji[emoji16]
 
Kuna siku natoka Dom kwenda Arusha nimekata Shabiby. Siku hiyo nililala kahoteli flani kako karibu kabisa na ofisi za Shabiby sikakumbuki jina.

Bus lilikua linaondoka saa 1 kamili, picha linaanza nimeshtuka usingizini saa 1 kasorobo! Kwanza sikuamini macho yangu manake mi huaga mwepesi sana kuamka mapema. Aisee nilikurupuka, tupia manguo kwn begi, piga mswaki huku navaa. Nilitoka mkuku pale hotelini hata sijaaga. Mbio mpaka Shabiby nimefika saa 1 kasoro 5 sioni bus! Nauliza jamaa pale nje wananiambia mbona bus limetoka mda tu? Nikadata!

Ila nikatuliza akili nikasema mimi sikimbizi bus, kama nimechelewa nachukua lingine. Nikaingia mule ndani ofisini nikawafata wale wadada kuwaonyesha ticket na kuuliza vizuri wakaniambia tulia boss bus limechelewa kidogo linakuja soon. Ndio nikapumua
[emoji23][emoji1787][emoji28][emoji38][emoji16][emoji1][emoji2][emoji3]
 
Back
Top Bottom