Je, hili linaweza kuwa tatizo gani la saikolojia?

Je, hili linaweza kuwa tatizo gani la saikolojia?

mtetezi12

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
24
Reaction score
138
Hivi ili linaweza kuwa tatizo gani la saikolojia?

Mtu kuwa uuongo sana yaani anadanganya kupitia kiasi. Kushindwa kujitambua ( yaani kuwa mtu ambaye anashindwa kudadavua mambo yake mwenyewe au kujisimamia )

Kuwa mtu mwenye wivu wa kupita kiasi, Mchonganishi, Mpenda sifa sana na kuongea kupita kiasi, Na mvivu kupita kiasi
 
Kuna ndugu yangu naishi naye ana matatizo ya saikolojia
Toka mwaka jana tulikutana na polisi kuongelea kuhusu kesi yake
Yeye pamoja na wazazi wangu walipotoka kijijini kwetu mke wake na watoto wake wanaishi south afrika
Mateso yake mpaka leo bado yanamsumbuwa tumejaribu njia zote lakini maisha yake bado ni yale yale tu hakuna chochote ambacho kimebadirika kwangu na kwa familia yake
Mpaka ndugu zake wameanza kuchoka na hali hiyo
Naombeni msaada wenu ndugu zangu

Maelezo yote haya lakini bado hujabainosha tatizo...

Hebu rudia tena taratibu kusoma ulichoandika...
 
Ninaishi na ndugu yangu mmoja kwasasa ana umri wa miaka 35
Mwaka mitatu nyuma apo aliachana na mke wake akaenda kuoa mwanamke mwingine uko kwa bahati mbaya uko nako akaachana na yule mwanamke
Ila uyu ndugu yangu moja ya tatizo yake kubwa ni mtu muongo sana yaani ana tatizo la kudanganya na anaga aibu wala nini anaweza kukosea the some mistake mara zote bila hata kujifunza
Pamoja na na hayo yote tatizo lake lingine ni mtu ambaye anajifanya mjuaji sana hashauriki wala nini , mvivu kupita kiasi
Pamoja na yote haya kipindi cha nyuma hapo alikuwa kidogo anajitambua
ILa kwasasa hali hiyo imeongezeka
Kwasasa hana pakulala amepoteza document zake zote
Tukijaribu kumshauria kuhusu kumsaidia hakuna tunachokipata kwake zaidi ya kutudanganya tu
Anajua kuwa tunajua anadanganya but bado anadanganya
Kwa kifupi nini inakuwa chanzo cha mtu kuwa muongo sana kupita kiasi na kushindwa kujitambuwa
Hiyo ndio Living Mechanism yake, nyir mnamuona amechanganyikiwa lakini anawatafuta mdogo mdogo😂😂
 
Hivi ili linaweza kuwa tatizo gani la saikolojia
Mtu kuwa
Muongo sana yaani anadanganya kupitia kiasi
Kushindwa kujitambua ( yaani kuwa mtu ambaye anashindwa kudadavua mambo yake mwenyewe au kujisimamia )
Kuwa mtu mwenye wivu wa kupita kiasi
Mchonganishi
Mpenda sifa sana na kuongea kupita kiasi
Na mvivu kupita kiasi

Pengne ni mwanaume.

Kama ni mpenz wako na anafanya Hayo mbele yako tu na ukaona yanapita ile Kiasi jua anajishtukia na hajiamini.

ila kama anafanya kwa watu wengne jua kuna tatizo kubwa zaid.
Na anahisi watu wanamuona tofauti na anataka kujionyesha tofauti.

Hizo ni dalili kuwa hayuko sawa in mental behavior .
Anaweza akawa na Anxiety, Depression au Bipolar disorder.

Unajua Mavitu /dispointment kwenye maisha zipo na kila mtu kwa wakat wake atapitia. Ila kuna wengne wakipitia wana over do baadhi ya vitu kwa kuhisi watu wanajua au wanawashangaa na ndio inapelekea wao kuact/kufanya vitu kupita kiasi wakijua wana weka uwiano kumbe wako way far frm Balance.
 
Swali zuri sana… na linaonyesha unajaribu kuelewa mambo kwa kina, si kuhukumu tu. 👍


Tabia ulizotaja zinaweza kuonekana kama “tatizo la saikolojia”, lakini ukweli ni kwamba si kila tabia mbaya ni ugonjwa wa akili. Wakati mwingine ni malezi, mazingira, uzoefu wa maisha, au tabia iliyojengeka kwa muda mrefu.


Hebu tuangalie kidogo kitaalamu 👇




1️⃣ Kudanganya kupita kiasi​


Kuna kitu kinaitwa Pathological lying
Hii ni hali ambapo mtu hudanganya mara kwa mara hata bila sababu kubwa.
Mara nyingi huambatana na:


  • Kutaka kuonekana bora kuliko alivyo
  • Hofu ya kukataliwa
  • Kujilinda kwa uwongo

Lakini mara nyingine ni tabia tu iliyojengeka.




2️⃣ Kushindwa kujitambua / kujisimamia​


Hii inaweza kuhusiana na:


  • Kujithamini chini (low self-esteem)
  • Kutokuwa na emotional maturity
  • Au matatizo ya ukuaji wa utu

Watu wengine hukua bila kufundishwa kuwajibika, hivyo wanakuwa wazito kujisimamia.




3️⃣ Wivu uliopitiliza​


Wivu mkali unaweza kuhusiana na:


  • Hofu ya kupoteza
  • Kutokujiamini
  • Au hata hali kama Delusional jealousy (ingawa hii ni hali kali zaidi sana)



4️⃣ Mchonganishi + Mpenda sifa kupita kiasi​


Hapa kuna tabia zinazofanana na sifa za:


  • Narcissistic personality disorder
  • Au wakati mwingine Histrionic personality disorder

Lakini kumbuka: kuwa mpenda sifa pekee haimaanishi mtu ana ugonjwa. Lazima tabia iwe:


  • Inajirudia sana
  • Inaharibu mahusiano
  • Inasababisha madhara makubwa



5️⃣ Uvivu kupita kiasi​


Hii si lazima iwe uvivu. Wakati mwingine inaweza kuwa:


  • Msongo wa mawazo (depression)
  • Kukosa motisha
  • Au kukata tamaa ndani kwa ndani



Muhimu Sana 💡​


Ili kuitwa “tatizo la saikolojia”, lazima:


  • Tabia iwe ya muda mrefu
  • Iwe inaharibu maisha ya mtu au watu wanaomzunguka
  • Na ichunguzwe na mtaalamu wa afya ya akili



Nikuulize kitu kidogo (si lazima ujibu kwa undani):
Hizi tabia unaziona kwa mtu fulani maalum? Au unajiuliza kwa ajili ya kujifunza tu?


Na kama zinakuathiri wewe moja kwa moja, naweza pia kukusaidia jinsi ya kukabiliana nazo bila kuumia sana.

.....KWA MSAADA WA Chat GPT...👆👆
NIMEIKOPI NA KUIPELEKA KULE KAMA ILIVYO.
 
Back
Top Bottom