Je, hili ni box la vidonge vya ARV?

Duh......ina maana kashavuka level ya kwanza tayari


Hapana , ni kwamba tiba ya ARV imepangwa kwa utaratibu wa first line ( yaani default treatment) then endapo kukitokea tatizo lolote kwenye first line hususani reason kubwa ya kuhama first line kwenda second line ni TREATMENT FAILURE ambayo wataalam lazima wajiridhishe kuwa kweli kabisa ni treatment failure ndipo mgonjwa anahamishiwa kwenda second line.

Mfano hata malaria, dawa mseto ya malaria kwa Tanzania ndio first line, yaani inaweza kutibu malaria kwa karibia 90% ya wagonjwa watakaoitumia na pia wagonjwa wengi wanaweza kuhimili zile ‘Side effects’
Ikitokea malaria ikaonekana ni positive kwa mgonjwa ndani ya wiki mbili au mwezi baada ya tiba ya dawa mseto ndipo mgonjwa huhamishiwa second line sasa ambayo pia kitaifa inajulikana ni DUO COTEXIN na wanafamilia wenzake kama ARTEQUICK NA ARTEQUIN

ni matumaini yangu mkuu umenielewa hapo kwenye habari ya first line na second line kwa mfano hai wa malaria.
NAWASILISHA.
 
Hiyo second line inatumika baada ya kwanza kufail au inakuwaje Mkuu.
Kama first line unapata side effect nyingi na kubwa..then inabidi upewe second line..bongo first line ni TLE
 
Asante mkuu...... kuna mdau wasapu ananiambia hizo ni PEP je ni kweli?
 
Nikijihisi malaria tu huwa nakimbilia DUO COTEXIN kumbe nakosea ehee, nimejifunza
 
Ndiyo unapima Mkuu kama unaijali afya yako.

Ushauri mzuri nadhani ni kutumia kinga sababu mtu anaweza pima leo yuko fresh ukajiachia na kumbe maambukizi kapata jana au juzi, pia anaweza pima leo yuko fresh kesho kaukanyaga kwa mtu mwingine we kesho kutwa mnakutana kama kawa ukijua ni mzima.

Life is full of betting aisee... usione kupima ni ujanja tumia kinga
 
Hiyo second line inatumika baada ya kwanza kufail au inakuwaje Mkuu.

Yes mpaka kuwe na treatment failure mkuu ambayo inaweza kuwa
1. Immunological failure ( kama allergic reaction baada ya kutumia dawa, hapa nazungumzia intolerable reactions kabisa)
2. Virological failure, yaani idadi ya vijidudu haipungui japokua mgonjwa anameza dawa
3.clinical failure hapa kuna mengi kitaalam ambayo nitaandika hata siku nyingine

Ila pia kuna toxicity ya dawa maybe ni mjamziti inabidi abadilishiwe from first to second line
 
Wapime na watumie kinga.

Wengi huwa wanatumia kinga mwanzoni mbele ya safari wanaacha.
 
Asante mkuu...... kuna mdau wasapu ananiambia hizo ni PEP je ni kweli?


Kwamba alijikuta kwenye mazingira ambayo yalipelekea kuchanganyika kwa damu na mtu anaedhaniwa kuwa muathirika ndio akatumia hizo kujiepusha na maambukizi?
 
Shukrani kwa ufafanuzi.
 
Nikijihisi malaria tu huwa nakimbilia DUO COTEXIN kumbe nakosea ehee, nimejifunza

Hujakosea mkuu, yaani kuna vigezo vingi saana kusema hii ni first line
Mseto uko affordable kwa kila mtanzania wizara imesema mseto iwe first line kwa sababu pia ili dawa iwe na sifa ya kuwa first line lazima kila mtu awe na uwezo wa kuinunua dawa.
Hizi ni taratibu za ki- sera tu
Duo cotexin haiko affordable kwa kila mtu japo ina uwezo mkubwa sana kutibu malaria ndio maana iko second line
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…