Je hili ni kweli?

Je hili ni kweli?

Nikikumbuka kile ulichokisema kwenye ule uzi wa akina baba ninakuelewa kabisa na kamwe huwezi kutamani.

me huwa nasema, kama kweli walifanyaga utafiti wakagundua kuwa asilimia kubwa ya wasichana hupenda wanaume kama baba yao, basi me nina fall kwenye hiyo asilimia iliyobaki.

labda sifa nayopenda ambayo baba anayo ni weupe tu. 😀
 
Na mada yangu ililenga wale baba kweli sio sperm donners!!

Inategemeana kwa kweli, kuna wababa wanaitwa baba kwasababu tu walituzaa watoto.Kwa wamama vilevile.
Baba huyu au mama huyu unakuta anatabia ambazo hutamani hata mtoto wako kuzirithi.

Ambacho hua natamani, ni walau mwanangu(wa kike) awe na tabia kama zangu hata robo tu.
 
Mama yangu ndio the best woman duniani lakini sijawahi kufikiria kuoa mwanamke anayefanana naye.

Ndoto yangu ilikuwa kuoa mke na kwahiyo lazima awe a unique being.

Kuna hatari kubwa ya kumlinganisha mke wako na mama yako. Hawa ni watu wawili tofauti na kila mmoja ana umuhimu wake kulingana na roles zake kwako. Kumbuka mama yako sio Saint au malaika. Mama anaoneka mzuri kwako kwasababu image anayoiproject kwa mtoto wake ni maalumu na tofauti kabisa na ile anayoionyesha kwa mume na watu wengine. Mama anaonyesha her best side kwa mtoto wake na kwa watu wengine wanapata na ile poisonous part. Siajabu mama yako has been a terrible wife kwa baba yako lakini anavumilia na kumfichia aibu.
This is a point maana Kuna wengine hawataki kuolewa na watu ka baba yake
 
Mimi napendana sana na binti wangu.
Lakini anasemaga hapendi mwanaume mlevi kama mimi baba yake. Na cha ajabu anatamani kua na mwanaume mwenye upendo wa dhathi kama mimi baba yake.
Sasa.......
Misijui hapa inakuaje
 
Mi ningependa kuolewa na mwanaume mwenye tabia za daddy angu kuanzia upole, tabia hekima akili hata physical appearance urefu yani everything
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Nimejikuta nacheka sana
 
Habari zenu wana JF?

Kuna usemi kuwa "wanawake hupenda kuolewa na baba zao" na "wanaume hupenda kuoa mama zao"

Dont get it wrong, ila ni kuwa binti huwa karibu sana na baba yake hivyo kupelekea kupenda kuwa na mume kama baba yake, halikadhalika kijana kuwa karibu na mama yake hupelekea atamani kuwa na mke kama mama yake (kwa sifa).

Sasa wapendwa wana JF naomba niwaulize, je kwa wanaume wewe ungetamani mke mwenye sifa za mama yako na kwa wanawake wenzangu, je ungetamani mume mwenye sifa kama za baba yako?

Niwatakie jioni njema.
Dada shemeji.....nmekumiss mnoo....!
Ulikuwa wapi
 
Si kwa kupotea huku, itabidi unilipe fidia kwa kukumiss...lol

Nimependa hii, lakini naona wengine tunapenda wenza waliofanana na baba baadhi ya vitu si vyote. Mfano wangu ni kichwa na height.
Hahahaaaa! Hebu ngoja nifikirie ninachokipenda Mimi.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Back
Top Bottom