Je hili ni kweli?

Je hili ni kweli?

Mazingira ya mtoto vile anavyokulia tangu kipindi cha utoto wake, inamuingia akilini kidogo kidogo kwa jinsi anavyoona anavyolelewa na watu wanavyoishi na kujifunza kutokana na kuwaona au kuwasikia kila siku(mara kwa mara).

Ukipata bahati ya kulelewa na bibi na babu utatamani na wewe ndoa yako uwe kama babu anavyompenda bibi mpaka uzeeni, busara, utu, heshima na kupenda majirani na kusaidiana.

Vile vile romantic movies, love stories, masupastaa, mama na baba, kaka na dada, majirani zenu, wazazi wa rafiki bora na maisha ya mwalimu, mchungaji au sheikh.

Ikiwa mtoto amelelewa katika mazingira ya dini pia inaweza kupelekea kupenda kuwa na mume mwenye imani kama mafundisho ya dini yanavyosema mfano wa tabia za mitume na maswahaba(wafuasi) wake.
 
Habari zenu wana JF?

Kuna usemi kuwa "wanawake hupenda kuolewa na baba zao" na "wanaume hupenda kuoa mama zao"

Dont get it wrong, ila ni kuwa binti huwa karibu sana na baba yake hivyo kupelekea kupenda kuwa na mume kama baba yake, halikadhalika kijana kuwa karibu na mama yake hupelekea atamani kuwa na mke kama mama yake (kwa sifa).

Sasa wapendwa wana JF naomba niwaulize, je kwa wanaume wewe ungetamani mke mwenye sifa za mama yako na kwa wanawake wenzangu, je ungetamani mume mwenye sifa kama za baba yako?

Niwatakie jioni njema.

Swali zuri sana hili mpendwa. Katika maisha mimi huwa naamini kuwa hakuna binadamu aliyekamilika. Kila binadamu ana mapungufu yake; Hivyo hata mama yangu pamoja na mema na mazuri yote aliyonayo, naye pia ana mapungufu yake.

Ni kweli, kuna tabia ambazo ningetamani sana mwanamke ambaye atakuja kuwa mke wangu awe nazo ila si zote kwa sababu kuna tabia pia ambazo mama yangu anazo ambazo sizipendi na ambazo nisingependa mke wangu aje kuwa nazo.
 
Swali zuri sana hili mpendwa. Katika maisha hakuna binadamu aliyekamilika. Kila binadamu ana mapungufu yake; Hivyo hata mama yangu naye ana mapungufu yake.

Ni kweli kuna tabia ambazo ningetamani sana mwanamke ambaye atakuja kuwa mke wangu awe nazo ila si zote kwa sababu kuna tabia pia ambazo mama yangu anazo ambazo sizipendi na ambazo nisingependa mke wangu aje kuwa nazo.
Good.
 
Back
Top Bottom