Je, hili wazo langu la biashara lipo sahihi?

Je, hili wazo langu la biashara lipo sahihi?

Msumb

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2022
Posts
3,452
Reaction score
5,372
Mambo vipi wana jf habari zenu mko poa nyote, natumaini hamjambo? Sasa twende kwenye jambo langu?

Nipo nimewaza sehemu nilipo mkoani hapa nimewaza biashara ambayo nimeona kwa hapa kama itanifaa hivi.

Nichukue kama kiduka hivi kidogo, harafu humo ndani niweke vinywaji kama pombe aina ya ambiance/ 5gin zinapatikana kwa wingi huku na vinaenda sana, niweke maziwa mgando/fresh, juisi, maji ya kunywa madogo na makubwa, pamoja na sigara,

Ila pombe niweke za tofauti tofauti kama konyagi, kvant, value, nk. Vipi wazo langu hapo maana sina mtaji nami najitafuta tu ila hii mtu yoyote anaweza weka inaenda sana.

Nimewakilisha kwenu
 
Mambo vipi wana jf habari zenu mko poa nyote, natumaini hamjambo!? Sasa twende kwenye jambo langu!?

Nipo nimewaza sehemu nilipo mkoani hapa nimewaza biashara ambayo nimeona kwa hapa kama itanifaa hivi,

Nichukue kama kiduka hivi kidogo, harafu humo ndani niweke vinywaji kama pombe aina ya ambiance/ 5gin zinapatikana kwa wingi huku na vinaenda sana, niweke maziwa mgando/fresh, juisi, maji ya kunywa madogo na makubwa, pamoja na sigara,

Ila pombe niweke za tofauti tofauti kama konyagi, kvant, value, nk. Vipi wazo langu hapo maana sina mtaji nami najitafuta tu ila hii mtu yoyote anaweza weka inaenda sana,

Nimewakilisha kwenu
Je hiyo biashara unaijua ya vinywaji vya pombe, wapinzani wako ni wakina nani kwenye hilo eneo na nguvu zao zikoje ama mapungufu yao yakoje kwa kujipambanua nawewe, wateja wao ni akina nani na wanaishi wapi, kumbuka wateja wa pombe ni walewale umejipangaje kwa hilo jibu haya kwanza tutaendelea
 
Ni wazo zuri ila lzaima kwanza ujue Nguvu ulionayo, madhaifu,fursa iliokuzunguka na vitisho vya upinzani pindi ikitokea
 
- Usiweke bidhaa yeyote mbayo inaharibika ndani ya siku chache. Jikite zaidi kwenye bidhaa ambazo hazihalibiki.

- Pombe ni biashara nzuri. Ukiwa na usimamiaji mzuri, Haina hasara.
Ndo nilikuwa na wazo ila sijaanza bado, kama kusimamia naweza kusimamia mwenyewe ikiwezekana
 
Je hiyo biashara unaijua ya vinywaji vya pombe, wapinzani wako ni wakina nani kwenye hilo eneo na nguvu zao zikoje ama mapungufu yao yakoje kwa kujipambanua nawewe, wateja wao ni akina nani na wanaishi wapi, kumbuka wateja wa pombe ni walewale umejipangaje kwa hilo jibu haya kwanza tutaendelea
Ndo lilikuwa ni wazo tu sina a z
 
Ndo lilikuwa ni wazo tu sina a z
Unapotaka kuanzisha biashara yoyote ile lazima uijue kwaundani ama kwakujifunza na kufanya utafiti wa soko kwa eneo husika, wapinzani, wateja, elimu yako ya ujasiriamali,changamoto (market research analysis)
 
Back
Top Bottom