Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya Woga, Kutasaidia?!.

Kwa maana nyingine unataka Rais aache kufanya haya anayoyafanya ili yaendelee kuwepo wakati anaweka misingi ya kwenye katiba ya Warioba.

Kumbuka pia hata Rais Ibrahim Lincoln aliweka misingi ya uongozi Marekani wakati huo huo akifanya kazi katika msingi wa Management by wandering around.
 

Sijui mwenzangu unaongelea procedure gani ambazo hazipo miaka 55 iliyopita ili tukae chini kuzidevelop. Mambo ya business as usual, kwenda kazini kusogoa na kunywa chai na kusoma magazeti ya udaku yamedumaza utendaji. Imefikia watu hawajui duties na responsibilities zao, na wengine hawako competent na vitendea kazi.

Mfanyakazi wa umma fanya kazi, chukua hatua, ongeza ujuzi hujui ni lini JPM atafanya ziara ya kushtukiza ofisini kwako.


Aangalie systems na procedures mara ngapi. Mipango, sera na taratibu zipo, tena nzuri tu na hilo halina ubishi. Tatizo watu hawazijui kwa vile hawapendi kuongeza maarifa kwa kujisomea yanayojiri na yanayohusu kazi na utendaji kazi.

Rais ana haki na hawajibiki kuomba ruhusa au kumwarifu mkuu wa kitengo taarifa ya kuzuru ili uandaliwe utaratibu wa kumdanganya na kuficha hali halisi. Kwa mfano ilifikia wakati wakuu wa mikoa na wilaya kufanyia matengezeno barabara na miundo mbinu mingine muhimu wakipewa taarifa ya mmoja wa viongozi wakuu wa nchi kufanya ziara mkoani au wilaya au kitengo husika. Kiongozi akipita anaona kila kitu kiko sawa wakati ni funika kombe mwanaharamu apite! Short term solution. Ikinyesha mvua siku moja baada ya kiongozi kumaliza ziara tatizo linarudi back to square one na pesa nyingi zimeshatumika!

Tufanye kazi kwa uadilifu, kuwajibika, ubunifu, kufuata taratibu na mipango iliyowekwa. Ifike wakati rais akitembelea ofisini kwako badala ya kuogopa ufurahie ugeni mkubwa.
 
Je watu wanazijua ports of entry za usafiri wa anga nchini? Je wajua kuwa ukipata access kutoka Mbeya, pale Dar terminal one unaweza kupeta tu?.
Jamaa kauliza...kwanini hamjiulizi kwanini yeye kaenda pale!
 
Mkuu Pasco huyu jamaa wa kukurupuka tayari nchi imeshamshinda na kwa kuwa ni mtu asiyeshaurika kwa kujiona anajua kila kitu basi nchi ndiyo inazidi kwenda mrama. Mama Samia kishaanza kumpinga kinamna na huku kukurupuka kwake (Kutumbua majipu)

Samia awataka waiga utumbuaji kutenda haki


 
Uko sawa Mkuu na Mama Samia kishaanza kumpinga huyu na kukurupuka kwake.

 

Yaani, katika utimamu wa akili kabisa unasema ni "heri ukose nidhamu kwa vile utafukuzwa kazi" kuliko kuwa na nidhamu? Mtu mwenye nidhamu ya woga anaweza kukiuka maadili lakini mwenye woga wa nidhamu atajitahidi kufuata maadili na weledi. Hakuna uzuri wa kuwa na mtu asiye na nidhamu.
 
kweli kazi ya Rais ni nzuri ila kwenye ufisadi na wizi hapo bado sana
 
Kuna kazi nyingine awaachie mawazir Na manahibu wazir wake waulize wapewe majibu ya kitaalam kwenye kamera siku zote mkubwa akikosea atasema usiniongopee kuna vitu alikuwa anapewa majibu tofauti kwa kuwa wafanyakazi waliona ni sahihi kuwa pale watu kutokaguliwa kwa kuwa wasafiri Wa ndani wanaposhukia ni sawa eti ubungo iwekwe scanner ya kukagua mizigo
 
Ni wale wa kuzungusha mikono na waliolamba matapishi yao kwa kuwakumbatia mafisadi papa ambao waliwatuhumu na kuwatangaza hadharani.
 
Wewe ni mnafiki tu.

Leo umemkubali Zitto na hoja zake wakati kwenye hansard ya Jamiiforum kumejaa matusi na kejeli ulizokuwa unamrushia kila mara ukisema ni muongo, mnafiki na ndumila kuwili.

Hii nchi ina watu wa ajabu kweli.
 
Mwanakijiji,heshima kuu kwako.
Bado natafakari hii U turn uliyofanya.Ulikuwa role model wetu kwa kusifia na kukosoa ikibidi lakini this time ni kusifia tu.
Nchi ilifikia pabaya,yes!!Wote tunakubali.Nidhamu ya utendaji ilishuka pia wote tunakubali.
Tunahitilafiana pale ambapo tunajenga mfumo wa Rais kuwa kila mahali,kwa ukweli na bila unafiki hatutafika na dalili zimeonekana hata hiyo jana.
Ni wazi kuna informers wanaompa taaarifa lakini nahisi ni mfumo ambao sio endelevu.Ikiwa Rais anaamini taasisi kama TISS imeoza,aifumue lakini asijenge TISS ingine ambayo inafanya kazi hata bila Chande kujua!!
Tumeona Makonda akimshtaki Mkurugenzi wa jiji kwa Rais badala ya kwa waziri wa Tamisemi,hii si sawa.
Lakini jana tulitegemea Rais atimue watu ati the spot na haikutokea na najaribu kuwaza tu,hivyo huko ujenzi hakuna majipu?
 


Wewe una utaalamu gani wa Management?
 
Private sector zinaendelea na kupata faida bila hiyo wandering management.Mo Dewji hawaendi kila na mahali na kushtukiza,hata Bakhresa lakini wanafikia malengo walijiwekewa.Tanzania tuna mfumo bora mno ambao unahitaji just a small push na mambo yaende.Chini kabisa ni mtaa au kitongoji ambacho kina mwenyekiti,kuna kijiji ambacho kina serikali,kuna kata,tarafa,wilaya na mkoa na kote serikali imefika.Na kuhakikisha kuwa kuna effective mechanism ya accountability.
Mkapa aliinyosha nchi na kujenga uchumi bila kushtukiza.
 
Wewe ni mnafiki tu.

Leo umemkubali Zitto na hoja zake wakati kwenye hansard ya Jamiiforum kumejaa matusi na kejeli ulizokuwa unamrushia kila mara ukisema ni muongo, mnafiki na ndumila kuwili.

Hii nchi ina watu wa ajabu kweli.

Hebu pevuka mkuu, hivi hujui kama kwenye siasa huwa hakuna adui wa kudumu, wala rafiki wa kudumu?
Hujui kama Mbowe na Kingunge ni marafiki? Na ina maana hujui kama Mbowe na Slaa sio marafiki kwa sasa?

Ova
 
Ajabu sifa kuu ya nyumbu ni kutonyumbulika. Wako static kimawazo. Wanasubiri nyumbu mkuu apunge mkono wafuatishe. Pathetic!
 
International arrivals ni muhimu kupita kwenye scanner.
Hapa Bongo utaratibu wao kutenganisha abiria wa nje na ndani ukoje?

Pasco unaposema "Kama hakuna scanner kwenye arrival zote duniani" umeshapita airport zote duniani?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…