Je, Houth ndiyo waliokata nyaya tatu za intaneti chini ya bahari ya Red Sea?

Je, Houth ndiyo waliokata nyaya tatu za intaneti chini ya bahari ya Red Sea?

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kuharibika kwa nyaya tatu za intaneti za chini ya bahari kumetajwa kuathiri karibu robo ya data za intaneti kwa maeneo ya mashariki ya kati,Ulaya na maeneo ya Asia.

Kukatika kwa nyaya hizo kumepelekea kizaazaa kwa wasambazaji data hizo ambapo wamelazimika kuzichepusha njia karibu robo ya data hizo kuziingiza kwenye nyaya na mifumo mingine ya usafirishaji data.

1709565083598.png

Three underwater data cables through the Red Sea are cut amid Houthi rebel attacks in the area

Red Sea cables have been damaged, disrupting internet traffic

 
Wanayo yafanya hayo magaidi kamwe hayatawasaidia wapalestina.
 
Tanzania tunashindwa nini kuwa na source yetu ya kuzalisha internet ?
Intaneti ni mawasialiano ya dunia nzima.
Tutakuwaje na intaneti yetu.
hIzo nyaya tatu twaweza tusiathirike nazo kwani nadhani sisi tunapata mkonga kutoka Afrika kusini ambao unaunganishwa na Ulaya na Marekani bila kupita red Sea
 
Ni ujinga wa hali ya juu kabisa Nchi ambazo wanaziadhibu ni za Kiafrika na Asia.

Wanazidi kuyafanya Maisha yawe magumu.
 
Ni ujinga wa hali ya juu kabisa Nchi ambazo wanaziadhibu ni za Kiafrika na Asia.

Wanazidi kuyafanya Maisha yawe magumu.
Hapo bado hajatuadhibu sisi.Amewaadhibu wale wale wanaohusika moja kwa moja
Si unaona JF bado iko hewani.
 
Hapo bado hajatuadhibu sisi.Amewaadhibu wale wale wanaohusika moja kwa moja
Si unaona JF bado iko hewani.
Wakati Waarabu wa Saudia walipoongeza Bei ya Mafuta na kupunguza uzalishaji wa Mafuta wakati wa vita ya Ukraine lengo lao lilikuwa ni kutuadhibu SISI walaji wa chini Masikini.

Kama Ndugu zao wanapigwa kwanini kwanini Waarabu wote wasiende huko Vitani.
 
Back
Top Bottom