Je, hukumu ya Sabaya imetolewa ili kuzima malalamiko ya mamilioni ya Watanzania kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Najua kuwa hii hukumu imekuja ghafla, kwa kuwa wananchi walikuwa wameshatangaziwa hapo kabla kuwa hukumu hiyo ya rufaa, ilikuwa imepangwa kutolewa tarehe 31 mwezi huu.

Sasa ninachojiuliza, ni kitu gani kilichofanya Mahakama irudishe nyuma,na kutoa hukumu, kabla ya tarehe ambayo ilikuwa imepangwa?

Timezoea kwa Mahakama zetu kusogeza mbele tarehe ya kutoa hukumu, hata zaidi ya mara moja.

Sasa ni kitu gani kilichosababosha hukumu ya Sabaya irudishwe nyuma, kitendo ambacho hukijazoeleka?

Pengine yasemwayo mitaani, tunaweza kuanza kuyaamini, kuwa hukumu ya Sabaya imerudishwa nyuma, Ili kuweza kuzima mjadala moto kweli kweli wa upandishwaji wa bei ya mafuta, ambao umeleta taharuki kubwa nchi nzima.
 
Kama kweli wamefanya hivyo watakuwa wanajidanganya tu, maumivu ya kupanda bei ya mafuta yanamuumiza mtanzania wa kawaida kila siku, hili la Sabaya ni kama upepo tu litapita.
 
Zaidi ya Watanzania asilimia 90 hawamjui Sabaya, na hata tunaomjua, kushinda rufaa si issue kwetu ya kujadili sana maana alibambikiwa kesi na chadema na kutengeneza mashahidi wa uongo na leo wameumbuka. Issue ya mafuta iko pale pale
 
Kwan sabaya hata kama ametolewa kwa mchongo ndo bei za vitu zitashuka ama tatizo liko pale pale tu
 
Alaaniwe aliyesababisha utofauti wa Bei ya mafuta Kati ya ZANZIBAR na Tanganyika,Narudia tena ALAANIWE.

Siyo Muda mrefu tutamkumbuka JPM.
Kwa kweli inashangaza.

Inakuwaje Katika nchi moja, upande mmoja wa Muungano Zanzibar, wauze Petroli kwa shilingi 2,600

Huku Tanganyika tukiumizwa kwa bei isiyopungua 3,100?
 
Na bado juzi kati wametangaza kuongeza salary,mfumuko wa bei ni hatari sana kwa uchumi wetu hasa huu wa mchongo!
 
Alaaniwe aliyesababisha utofauti wa Bei ya mafuta Kati ya ZANZIBAR na Tanganyika,Narudia tena ALAANIWE.

Siyo Muda mrefu tutamkumbuka JPM.
Huyo ndiye aliyeharibu mifumo yote hapa nchini.Fikiria alivyosambaratisha sekta binafsi hasa kwa kodi kandamizi,ubambikaji kesi na kupora fedha za kigeni!Biashara nyingi zilifungwa na hakuna chochote kilichorekebishwa hadi sasa.Serikali yetu ni ya anasa kwa watawala huku wananchi wakibebeshwa kila gharama.
Leo kodi na tozo kwenye kila lita ya mafuta zinafanya bei kufikia hata mara mbili ya bei mafuta yanapoingia nchini.
Bila kukubali hali halisi tutabakia kusema bora marehemu angerejea duniani halafu tumrudishe kwenye urais wake.Tatizo letu ni mawazo mgando ya wanaccm,mlisema wapinzani wanawachelewesha!Hivi tumeshafika Harare?
 
Na bado juzi kati wametangaza kuongeza salary,mfumuko wa bei ni hatari sana kwa uchumi wetu hasa huu wa mchongo!
Je,kilichopandisha bei ya mafuta miaka hii 7 kulikuwa na nyongeza ya mishahara?Shida ipo kwenye utawala usio na huruma kwa raia wenzao.Tozo zimeongeza bei maradufu.
 

Aiseeeee
 
 
A call for reconciliation and reconstruction of the national unit🤸
 
Kwa kaisi kikubwa mtoa mada unaweza kuwa sahihi kabisa. Ndiyo njia wanasiasa huwa wanazitumia kubadili upepo.

Kitu kingine ni kuwa, hii hukumu ya leo si ya kushangaza sana hasa hasa ukiwa mfuatiliaji mzuri wa siasa za Bongo. Kingine ni kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa wahusika kufutiwa mashtaka kwa makosa yaliyobakia kwa ile mnachoita 'Mwendesha mashtaka hana nia ya kuendelea na mashtaka hayo'.

Mie kwa jicho langu, nadhani huyu ndugu alimkera Mama mahala hivyo ikabidi yafukuliwe mafaili yake. Ila hapakuwa na nia ya dhati ya kumshtaki kiukweli kweli.
 
Msoga style
Kipindi kile amekabwa na kashfa kibao wakaja na series ya babu wa Loliondo, ikawa ni habari inayopata coverage kubwa kwenye media zote, kila siku mawaziri wanapokezana kwenda kwa babu
 
Mleta mada anatudanganya Tofautisha kesi ile ya Rufani iliyosomwa leo Mahakama kuu na hiyo unayoisema mleta mada ya tarehe 31/05/2022, Mbele ya Mh. Kisinda ya Uhujumu uchumi.

Ungekuwa na hoja kama kesi ya Rufani Mahakama kuu ilikua isomwe tarehe 31/05/2022 lakini ikisomwa leo jambo ambalo si kweli.

You are misinformed and misleading people.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…