Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Najua kuwa hii hukumu imekuja ghafla, kwa kuwa wananchi walikuwa wameshatangaziwa hapo kabla kuwa hukumu hiyo ya rufaa, ilikuwa imepangwa kutolewa tarehe 31 mwezi huu.
Sasa ninachojiuliza, ni kitu gani kilichofanya Mahakama irudishe nyuma,na kutoa hukumu, kabla ya tarehe ambayo ilikuwa imepangwa?
Timezoea kwa Mahakama zetu kusogeza mbele tarehe ya kutoa hukumu, hata zaidi ya mara moja.
Sasa ni kitu gani kilichosababosha hukumu ya Sabaya irudishwe nyuma, kitendo ambacho hukijazoeleka?
Pengine yasemwayo mitaani, tunaweza kuanza kuyaamini, kuwa hukumu ya Sabaya imerudishwa nyuma, Ili kuweza kuzima mjadala moto kweli kweli wa upandishwaji wa bei ya mafuta, ambao umeleta taharuki kubwa nchi nzima.