Je, huu nao ni utapeli? Mniokoe kabla hakijanikuta kitu

Fabian Vitus

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
6,347
Reaction score
8,254
Katika pita pita zangu nimekutana na mdada mmoja yupo London kaniambia kanielewa na ana zawadi anataka anitumie hivo muhuni kutokana na matukio nimekutana nayo nikaona nimtajie jina lisilo langu ila nalitumia namba nikampa iliyo active.

Sasa kaniambia mzigo umekamilika na risiti kanitumia ila kaweka $3000 katika huo mzigo lakini sasa Masha bado yapo naomba msaada wa mawazo kabla, anasema kesho utakua umefika airport.
 
Asije akakutumia KA UGONJWA kwenye sanduku ili kupoteza wapenda mbususu kama mzabzab
 

Unatapeliwa kifala sana. Wakenya na Wanaijeria ndo michezo yao. Huo mzigo ili uupate kuna kiwango ataomba utume kwa shirika la ndege linalosafirisha au ofisi x na hapo ndo unaenda tapeliwa
 
mara utaambiwa mzigo umefika kenya...tuma hela wakusafirishie uje bongo....atakutumia hadi namba ya wakala ulipofika hapo kenya....hiyo ndo ramani watakayokupa...sasa hapo akili kumkichwa...tuma hela wakupige
 
Utapeli huo nilikutana nao mwaka 2011 nikiwa 1st year chuo. kumbe bado upo ?
 
Hebu acha tamaa za kijinga we kijana, utaambiwa mzigo umefika ila hauezi kutoka msaidie kulipia sababu ye yuko london hawezi, then atakupa number uwasiliane na mtu wa cargo airport then atakupa kiswahili unalipia faster ili ukienda kuchukua utakuta $3000 nawe umeamini kumbe ni matapeli na namba haitapatikana tena, kumbe bado tu huo wizi unaendelea na watu mnaibiwa?
 
Utapeli. Waliwahi kuja kwangu wakifikiri me ni ndezi. Nikawatolea uvivu
 

Attachments

  • Screenshot_20250606_160949_WhatsApp.jpg
    256.1 KB · Views: 27
🤣🤣 nikweli mkuu hata mimi amenitumia umeshafika
 
Hiyo ni kama milioni 7
Dah jamaa umeshatoka kimaisha hapo anzisha jiko zuri la kiepe yai utapiga pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…