Je huu ndio ukweli kuhusu BOT?

Je huu ndio ukweli kuhusu BOT?

Nafikiri hapa tuwe wakweli. Haya mambo kwa TZ yapo kila sehemu, mfano mdogo nenda pale SUA utakuta vijana wengi wanaoajiliwa ni watoto wa ma-prof. either wako kazini au walishastaafu, tena sio kazi za kufundisha tu hata kazi za kugawa mishahara. Kama sio mtoto wa mkubwa ni based on kabila--angalia MSOLLA muda aliokaa SUA na watu wa IRINGA walivyoongezeka pale--kwanza unaambiwa kuwa uki-contest kazi na mtu wa IRINGA wakati wa MSOLLA elewa kuwa umeshashindwa. I think waswahili wanasema mkono unajikuna unapoweza--so kama SUMAYE alikuwa PM anaweza kujikuna BOT ni kama kushika tumbo. So mimi sioni kipya hapa otherwise kama hawa vijana hawajasoma lakini kwa ELIMU ya TZ hawa watakuwa wamesoma shule zilizo bora ambazo baba zao kwa kutumia pesa walizoziiba serikali waliweza ku-afford kulipa FEES.

Ieleweke kwanza siku serikali hata kama wakitangaza kazi, hakuna system ambayo ni transparent inayojali fair competition. Na bora hizo kazi wanafanya watz, je nafasi walizonazo wanyarwanda/warundi na wengine mbona hizo vipi.

Semanao,

Niliwahi kufanya research ndogo miaka ya nyuma kuhusu ukabila kwa nafasi za kazi jeshini na kwenye bank. Wakati huo kulikuwa na
maneno mengi kwamba NBC walikuwa wanaajiriwa Wanyakyusa tu shauri ya Nsekela na jeshini Wakurya shauri ya akina Msuguri, Mwita na wengine.

Nilichogundua ni kwamba Wanyakyusa wengi walikuwa wanachagua kufanya kazi NBC wakiamini watapanda vyeo kirahisi. Hivyo hivyo Wakurya kule jeshini.

Makabila mengine ni watu wachache sana walikuwa wanaomba kazi NBC au jeshini kwa hofu kwamba huko kuna upendeleo.

Matokeo yake Wanyakyusa wengi walikuwa NBC na kukitokea vyeo basi chance ya mmoja wao kupewa ilikuwa kubwa kwasababu walikuwa wengi, hivyo hivyo na jeshini kwa Wakurya.

Wakati mwingine hii hofu inaweza kutupeleka pabaya mno. Sisemi NBC au jeshini hakukuwa na ukabila, ila idadi kubwa ya watu wa kabila moja ilitokana na hiyo dhana ya kuamini watapendelewa/hawatapendelewa.
 
bila ya shaka watoto wa wakubwa wengi wanavyeti vizuri kuliko hata hao wawalala hoi kwa vile wamesomeshwa nje ya nchi kwa mapesa mengi ama ya serikali au ya wazee wao waliyoyachota serikalini. all in all mara nyingi wamekuwa wakiajiriwa nafasi nyeti kwa kuwa wanavyo vyeti vyao.

tunachoongelea hapa sio hawa watu kuajiriwa kwa kuwa wana vyeti au la, kwa mfano ikiwa nafasi ipo moja, na sote tunavyo vyeti vya daraja sawa, nani anapewa kipa umbele wa kazi ile?

sitegei kama pamela lowassa anacheti kizuri mno kiasi cha kuwa kazi apate yeye asipate mwengine......au ndo tuseme kwa nafasi yake yeye aliomba kazi peke yake?

kila mtu na apewe haki yake anayostahili, akiwa mtoto wa mkubwa na mtoto wa mdogo bila ya upendeleo

ahsante
 
Thats warr am toking abaut!

Well said gaijin. Mfano wa mtoto wa Powel hapa US ulikuwa mzuri zaidi. Ni kweli mtoto wa Powell amesoma vizuri na ana vyeti bora tu. Ila uchunguzi ulipoanza kufanyika, ilionekana pia kuwa kuna watu wengine zaidi walikuwa na vyeti kama vyake na wengine hata kumzidi lakini wakanyimwa nafasi hiyo. Watu walivyoshika bango, mtoto wa Powell akaachia ngazi.

Tanzania napo ni the same. Mtoto wa Makamba ana elimu sawa tu na mtoto wa Mzakuki lakini mtoto wa Makamba anapata kazi ikulu na mtoto wa Mzakuki anaenda kufundisha Lindi!
 
ndiyo maana ukiangalia tatizo siyo ukabila hasa bali kile mwalimu alichokiita "undugunization" utaona watu wanaoajiriwa sehemu fulani fulani ni kutokana na undugu zaidi (hata wa kusingizia) kuliko kuangalia kabila moja. Familia yangu mwenyewe sasa ni kizazi cha tatu tuko ndani ya Jeshi la Polisi, na siyo kwa sababu ya undugu tena (ingawa mwanzoni bila ya shaka tulipoomba vinafasi tuliangaliwa majina yetu) lakini siku hizi ukienda kuomba kibarua wakiliona hilo jina tu wanauliza "unamfahamu so and so" .. u better say you do.. na stori zinapigwa na utatumwa "ukimuona mpe salamu zake".. na dili linakuwa limemalizwa hapo.
 
Nafikiri inabidi tuangalie system nzima ya hizi ajira kama kweli BOT/IKULU na govt. related organs kama wana kawaida ya kutangaza ajira, isije ikawa nafasi zinatengenezwa kwa kuwa kuna mtoto wa fulani kamaliza chuo.

Jaribu kufanya research kidogo kwenye vutengo vya serikali ambavyo vinalipa pesa nzuri, asilimia kubwa ni watoto wa wakubwa--waziri/katibu mkuu/ n.k. I dought kama hizi kazi uwa zinatangazwa. So mfumo mzima uko kisiri siri tu hakuna cha interview wala mtoto wa interview. Je tutafika? nafikiri Makwaia wa Kuhenga apewe topic ya kufanyia kazi.
 
Mimi ninawafahamu vijana watatu ambao wamesoma huku Europe wamepata kazi hapo BOT kwenye IT. Ni watoto wa wakulima.

Sijui walipataje ila wamepata. Walianza kazi sehemu nyingine na baada ya muda wakapata kazi pale baada ya hizo kazi kutangazwa. Naamini kilichowasaidia zaidi ni vyeti vyao.

Sijui kwenye maeneo mengine maana IT ilikuwa changa na pia ilikuwa na watu wachache wenye masters, hivyo hata competition ilikuwa ndogo.
 
ila mie nawajua kwenye hiyo list baadhi yao ni mazumbukuku...na mmoja nina uhakika hata form four hana cheti..lakini uko BOT
 
ila mie nawajua kwenye hiyo list baadhi yao ni mazumbukuku...na mmoja nina uhakika hata form four hana cheti..lakini uko BOT

Ni yupi huyo? Hakuna kuficha tena, inabidi kuwajua watu ambao tunadhani hawana sifa.
 
kwenye hiyo list kuna wengine wenye just if not less than 21 yrs..sasa ni vipi uwe na umri huo alafu uwe ushamaliza degree?hadi uwe na uzoevu wa kuajiriwa benki kuu?
 
kiswahili kirefu cha nini? HIvi ni nani atadirikia kutowapitisha hawa watoto endapo watagombea nafasi hizo na watoto wa mkulima.Tusidanganyane na kujaribu kujiliwaza hapa.Tanzania hakuna kupeana nafasi kwa qualification ni kujuana kwanza qualifications baadaye.Mtoto wa mkulima atapata nafasi endapo tu nafasi hizo zitakuwa ni nyingi.
 
Mtanzania,

Good points. Nilikuambia kuwa tunakubaliana zaidi ya tunavyotofauitiana. Hapa umesema ukweli kabisaaaa. Kama vigogo wanasomesha watoto wao na kuwapatia elimu yakutosha. Ni vigumu sana kushindanisha watoto wa vigogo na walalahoi.

Asante kwa hili.

mwafrika wa kike & Mtanzania

Ni sawa mnalolisema lakini kwa sasa halina nguvu sana. Mimi katika experience yangu ya Tanzania ya sasa hata watoto wa wakulima wana uwezo sana wamesoma.

Labda hawa watoto wa wakubwa wanachozidi ambacho pia kinatumika kama siasa ni kingereza tu.

wanaonekana kuwa wamesoma vizuri kwa sababu tu wanajua kuongea kingereza lakini hakuna kitu kinahitwa elimu baada ya kingereza (kwa kifupi utaalamu hakuna).
 
Back
Top Bottom