Nafikiri hapa tuwe wakweli. Haya mambo kwa TZ yapo kila sehemu, mfano mdogo nenda pale SUA utakuta vijana wengi wanaoajiliwa ni watoto wa ma-prof. either wako kazini au walishastaafu, tena sio kazi za kufundisha tu hata kazi za kugawa mishahara. Kama sio mtoto wa mkubwa ni based on kabila--angalia MSOLLA muda aliokaa SUA na watu wa IRINGA walivyoongezeka pale--kwanza unaambiwa kuwa uki-contest kazi na mtu wa IRINGA wakati wa MSOLLA elewa kuwa umeshashindwa. I think waswahili wanasema mkono unajikuna unapoweza--so kama SUMAYE alikuwa PM anaweza kujikuna BOT ni kama kushika tumbo. So mimi sioni kipya hapa otherwise kama hawa vijana hawajasoma lakini kwa ELIMU ya TZ hawa watakuwa wamesoma shule zilizo bora ambazo baba zao kwa kutumia pesa walizoziiba serikali waliweza ku-afford kulipa FEES.
Ieleweke kwanza siku serikali hata kama wakitangaza kazi, hakuna system ambayo ni transparent inayojali fair competition. Na bora hizo kazi wanafanya watz, je nafasi walizonazo wanyarwanda/warundi na wengine mbona hizo vipi.
Semanao,
Niliwahi kufanya research ndogo miaka ya nyuma kuhusu ukabila kwa nafasi za kazi jeshini na kwenye bank. Wakati huo kulikuwa na
maneno mengi kwamba NBC walikuwa wanaajiriwa Wanyakyusa tu shauri ya Nsekela na jeshini Wakurya shauri ya akina Msuguri, Mwita na wengine.
Nilichogundua ni kwamba Wanyakyusa wengi walikuwa wanachagua kufanya kazi NBC wakiamini watapanda vyeo kirahisi. Hivyo hivyo Wakurya kule jeshini.
Makabila mengine ni watu wachache sana walikuwa wanaomba kazi NBC au jeshini kwa hofu kwamba huko kuna upendeleo.
Matokeo yake Wanyakyusa wengi walikuwa NBC na kukitokea vyeo basi chance ya mmoja wao kupewa ilikuwa kubwa kwasababu walikuwa wengi, hivyo hivyo na jeshini kwa Wakurya.
Wakati mwingine hii hofu inaweza kutupeleka pabaya mno. Sisemi NBC au jeshini hakukuwa na ukabila, ila idadi kubwa ya watu wa kabila moja ilitokana na hiyo dhana ya kuamini watapendelewa/hawatapendelewa.