Ndicho walichotaka siku zote. Waliwaza wataingiaje DRC kuyachuma madini haya adimu na adhimu duniani? Kwanza wakamfadhili Rwanda ili kumchomganisha rasmi na jumuiya ya kimataifa. Wakampa effective equipment za kujilinda na mashambulizi ya anga. Kagame akavimba kichwa. Baada ya hapo mataifa wakaanza kumshushia lawama kwa kuivamia DRC wakamwekea vikwazo halafu sasa wameamua kuingia upande wa pili DRC ili rasmi wapewe migodi wachimbe wao wenyewe. Kumbuka walichotaka kwa Ukraine, Zelensiky akajifanya kukataa, lakini baadaye akaomba radhi na muda siyo mrefu atarudi Marekani kuitoa rasmi Ukraine kwa Marekani. Marekani ndiyo tatizo kubwa duniani. No peace with America but neo colonialism.