Je, huu ni Mwisho wa Messi na Ronaldo?

Je, huu ni Mwisho wa Messi na Ronaldo?

zagarinojo

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2020
Posts
2,622
Reaction score
2,846
Inaniuma sana nikiwa Kama shabiki wa soka mkubwa. Hasa nikiwatazama mahasimu wakubwa wa soka waliokuwa wakinogesha soka kwa uhasimu wao uliowekwa na mashabiki wa soka duniani?

Majina yao yamekosekana katika Tuzo za Uefa (Best Men's Player) katika hali isiyo ya kawaida. Ikiwa ni kwa mara ya kwanza toka 2010 majina ya aidha Ronaldo au Messi kukosekana kwenye Tuzo hizo. Majina yaliyotajwa yakiwa ni Kelvin De Bryune, Manuel Neur na Robert Lewandoski.

Nikiwa Kama shabiki wa soka kama kuna kitu kitaniuma ni kuona wanastaafu.Interest yangu kwenye soka inaweza kupungua kabisa kwa kuwakosa wawili hawa.

Itakumbukwa pia Tuzo za Ballon D'or mwaka huu hazitatolewa na mashabiki wa soka hawakupendekeza kabisa majina ya Messi Na Ronaldo.

Hii inatosha kusema Ufalme wa Nyota hawa bora kabsa Duniani umefika mwisho?

Je, Unadhani Dunia Itawahi kuwa na wachezaji bora Kama hawa Dena?
 
Ngumu sana kutokea aiseee! Ila nafurahi kuona ushindani wao kabla hawajastaafu!
 
Inawezekana wakatokea huko mbele ya safari...duniani hapa usije sema never.
 
Mnyama cr7 jeshi na mtu wa ajabu messi dah ile ligi yao sijui kama watatokea miaka ya hv karibuni kama hawa viumbe

Waliobaki hawa pisi kali neymar watoto wa mama.

Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom