Msolo
JF-Expert Member
- Oct 19, 2008
- 3,832
- 5,309
Za Weekend Wakuu!
Matoleo mapya ya simu tofauti katika miaka ya karibuni imenipa tafakari hii, kwamba hakuna features mpya kulinganisha na miaka ya nyuma kabla ya iOS na Android, na miaka ya mwanzo ya iphone 2007.
Je, unakumbuka enzi zile kila mtu alikuwa na simu tofauti na ya mwenzake, kila moja ikiwa na features za kipekee? Simu kama Nokia, Sony Ericsson, Motorola, Blackberry, na baadaye kidogo, ujio wa iPhone mwaka 2007, kila toleo jipya lilikuwa na kitu kipya cha pekee.
Leo hii, nani anaweza kueleza kwa uhakika ni feature zipi za kipekee kwenye kila toleo jipya la simu? Mara nyingi, hakuna mabadiliko makubwa.
Tumeifikia hatua ambapo ubunifu unaosifiwa kwenye toleo jipya la Samsung Galaxy S25 Edge kuwa nyembamba zaidi! Hapo zamani, hilo lisingetosha kuvutia watu.
Mimi binafsi nimeshatumia iPhone 3G, 5s, 6s, Huawei Nexus 6p, Samsung Galaxy S2, Pixel 2, Pixel 4a, na sasa Pixel 8a. Kwa maoni yangu, miaka ya karibuni hakuna jipya sana la kipekee kwenye smartphones, ni kama tumerudia mzunguko uleule kwa muonekano tofauti.
Wewe unakumbuka simu ipi ya zamani ambayo ilikuvutia sana na kwa nini?