Wanabodi,
Kwanza naomba kukiri kuunga mkono kwa dhati, juhudi zote na hatua zote zinazochukuliwa na rais Magufuli katika vita dhidi ya rushwa, ufisadi, wizi wa rasilimali zetu na kusimamia uwajibikaji, ila katika utekelezaji wa juhudi hizo, sometimes kunatokea hapa na pale utekelezaji huo ukafanywa ndivyo sivyo, yaani doing the right thing, and the right time, but not doing it right. Kwa vile rais Magufuli, licha ya kuwa ni mtu anayeitwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, a human being, anaweza kufanya makosa ya kibinaadamu, lakini pia yeye ni taasisi inayoitwa Presidential Institution, taasisi hii ni purported to be perfect, haiwezi kukosea, hivyo rais Magufuli anategemewa kuwa perfect by doing the right thing, at the right time and do it right!. Makosa yoyote madodo madogo ya kibinaadamu, yanaweza kuwa tolerated yakifanywa na mtu mwingine yoyote, but not our president.
Angalia kilichofanyika hapa.
https://www.instagram.com/p/BbKBCKpnqK0/
Isn't This Bullying and Intimidation?.
Kwa maoni yangu, this is bullying na intimidation. Kwa rais Magufuli yeye binafsi is very good in numbers, actually I think he is genius kwenye kutunza kumbukumbu za numbers za takwimu, namkumbuka jinsi alipokuwa waziri wa mifugo, kichwani kwake, alikuwa na idadi ya ng'ombe, mbuzi, tena nikasikia kuwa ana hadi idadi ya samaki wetu. Alipokuwa waziri wa ujenzi, alikuwa na figures za urefu wa barabara zote za Tanroad na zimejengwa kwa kiasi gani. Then rais wetu asitegemee kila kiongozi wa umma, atakuwa mzuri kama yeye kwa kukurupushwa tuu na kuulizwa figures, alafu ajibu kutoka kichwani.
Is This Fair?, Huu Sio Udhalilishaji?.
This is not fair, hii sii haki, hii ni some sort of intimidation na udhalilishaji wa kiongozi wa umma mbele ya public ya watu. Hizi intimidations niliwahi kuzizungumza hapa. Kusema ukweli, kuna vitu rais wetu huwa anavisema, havikupaswa kusemwa na rais, na kuna vitu anavifanya, havikupaswa kufanywa na rais, kama wasaidizi wake mpo, na mnaona, na imejiridhisha he is doing the right thing, hivyo wote tuendelee kumshangilia tuu rais wetu, kwa baadhi yetu sisi ambao ni wakweli daima, tunakua hatujitendei haki nafsi zetu, hivyo mwisho wa uwezo wetu ni kusema tuu, kwa sababu hizi bullying na intimidations kwenye madogo zikiachwa, mbele ya safari tutakushuhudia makubwa Zaidi, tukidhani ndio kumsaidia rais wetu kumbe tunamchoresha!.
Tumbua Tumbua, Ziara za Kushutukiza na Utoaji Nje Siri za Serikali.
Niliwahi kupinga utekelezaji wa baadhi ya Tumbua tumbua, na kulalamikia double standards. Kwenye ziara za kushtukiza, nikasema ni intimidating, hivyo kutajenga nidhamu ya woga, lakini pia nikapinga hii ya rais kusema chochote hata vitu ambavyo hakupaswa kusema kama disclosure of tapping telephone conversations, au kuwaanika secret agents etc, nilishauri
Marais Wengine Hufanya Vipi?.
Nikiwa ripota wa newsroom, nimewahi kushiriki ziara nyingi za rais za ndani ya nchi na nje ya nchi. Wakati rais akifanya ziara popote, wahusika wote watakaohusiana na ziara hiyo huarifiwa. Rais akiishawasili hufanyiwa briefing, na kila jioni hufanya postmortem, hivyo kuna mambo mengine ni mambo ya ndani kuuliza kule kwenye briefings, na sio kila kitu kuuliza mbele ya kadamnasi ya watu, huu ni udhalilishaji na kuaibishana.
A Way Forward.
Kwa vile rais wetu pia ni binadamu, naendelea kuwasisitiza wale wasaidizi wake, waendelee kumsaidia rais wetu, kutenganisha the two personalities, kati ya mtu anayeitwa Dr John Pombe Joseph Magufuli, na Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Dr. Magufuli anaweza kuwaza lolote, kufanya lolote popote, au anaweza kusema chochote popote, lakini Rais Magufuli, hawezi kufanya lolote or kusema chochote, he got to do only the right thing at the right time and do it right!.
Namtakia ziara njema.
Paskali