Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?

Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?

Ni ushenzi sana. DED huwezi kujieleza wakati wewe ndo key player hata meya anakuzidi? then unajitapa wewe ni kichwa, mtaalamu, really?
Huyo DED atakuwa wa chadema...juzi wakati wanateuliwa tuliwambia waache kuteuwana makada..
 
Paskali kulikuwa hakuna haja ya kuwavua madaraka kwa speed ya radi.
Kitu muhimu tena chenye tija ilikuwa kugundua tatizo kuwa wakurugenzi wote wawili hawakujibu oral exam ya raisi kama alivyotarajia,ilitakiwa kuandaa secular au mafunzo maalumu kwa wakurugenzi wa wilaya zote ili makosa kama hayo yasijirudie na huo ndio muarobaini wa tatizo
Lakini jambo la pili na muhimu ni kuleta mfumo wa QMS ya ISO kwenye tawala za mikoa itasaidia sana.Sio sahihi kila mkuu yeyote anakuja na mpya nje ya utaratibu
Hakuna haja ya kupoteza fedha za umma kufundisha watu majukumu yao...wakati wanateuliwa wana fursa ya kujipima na kutambua kuwa kama wataweza kasi hii au la.
Hakuna sehemu ya kusomea ukurugenzi mkuu!!
 
Hapa kazi tu.

Wakurugenzi hao wamejidhalilisha wenyewe,Halmashauri na mamlaka ya uteuzi.

Katika muktadha wa ziara ya kiongozi mkuu katika eneo lako haitarajiwi ukakosa data zote muhimu au maeneo mahsusi ya miradi iliyoletewa fedha na Serikali kuu.

DED kama accounting officer ana wajibu wa kujua kila senti iingiayo na kutoka halmashauri kwa kichwa kwani ni kazi yake ya kila siku na ni maswali anayoyajibu kwa wawakilishi wa wananchi au wananchi moja kwa moja.

Isitoshe mkurugenzi ana vikao vya kila juma au kila siku au kila mwezi vinavyombrief kuhusu maswala ya miradi ya maendeleo na fedha zinazotarajiwa kupatikana au zilizopatikana kutoka vyanzo vyote.yaani kuhusu fedha ya miradi kwa mkurugenzi ni sawa na sala ya baba yetu na muumini wa kikiristu.

Unapokuwa na mkurugenzi asitefahamu ni kiasi gani cha fedha za road fund zimefika kwenye halmashauri yake hutegemei kama ataweza kusimamia mradi wa barabara husika na mambo ndipo yanapokwamia na lawama au matusi yatarudi kwa mh Rais.

DED kama accounting officer aka afisa masuhuri wa halmashauri huandikiwa kwa barua kiasi cha fedha za mradi zinazoingia halmashauri sometimes days or weeks before disbursement ya hizo funds.

DED hupelekewa na mweka hazina statement au taarifa ya fedha yoyote inayoingia halmashauri.
Pia fedha yoyote inayoingia halmashauri hujadilowa kwenye vikao vya kamati za mipango na fedha na hatimaye baraz zima la madiwani ambalo katibu wake ni DED.

Kwa maoni yangu hakuna excuse ya DED kushindwa kujua figure ya fedha nyingi za mradi wa barabara zaidi ya kiwango kikuu cha uzembe.

Kama DED hajui ni kiasi gani cha fedha za mradi wa road fund ambayo ni nyingi how come anaweza kujua deni au fedha ya mtumishi(say nauli ya likizo) kama mdogo mfano mwalimu wa shule ya msingi aliyeko kwenye halmashauri yake???

Wakurugenzi hawa waneonesha kiwango kikubwa cha irresponsibility na wamestahili adhabu waliyopata.

Hilo ni funzo kwetu sote especially watumishi wa umma.

JPM ni no nonesense President, every subordinate must have known him better and therefore he/she should be super prepared .

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Jingalao nakuunga mkono kwa asilimia 100% . Kwa hili la Mkurugenzi kutojua kiasi kilichoingia huku akiwa pia signatory Ni ujinga mkubwa na ni indicator kubwa kuwa haijui JD yake.
 
Huyu Mama anasimamia;
Afya,
Elimu Sec,
Elimu Msingi,
Utawala,
Ardhi,
Kilimo,
Maji,
Mifugo,
Uhandisi Majengo,
Uhandisi Barabara,
Utamaduni,
Mazingira,
Fedha na Uchumi,
Mipango,
Maliasili, nk

Je anatakiwa kujua Kila Fungu lililoelekezwa humo??
Anatakiw kujua kama sala...anatakiwa kumjua mtumishi mmoja mmoja.
Kwa maoni yako tukimuuliza DMO kwa nini kituo flani hakitoi huduma flani ya afya ataanza kusema nina vituo 60 vya kutolea huduma kwa hiyo sijakariri??Siku mkuu wa hospitali akiulizwa umeletewa kiasi gani fedha za dawa atajibu mpaka niongee na mfamasia??Huo ni upuuzi uliokuweko huko nyuma sasa ni wakati wa kazi tu.
 


Naomba ieleweke kwamba sitetei wakurugenzi wa Bukoba kutumbuliwa kwa sababu sababu za kutenguliwa kwao sizifahamu.

Hoja yangu itajikita jinsi Rais Magufuli,naweza kusema navyowapelekesha viongozi majukwaani kwa maswali ambayo yanahitaji Takwimu ambazo mda mwingine kiongozi anaweza kutokuwa nazo kichwani

Case Study iliyotokea Bukoba leo sio jambo la kuacha lipite.

Kwa wasiofahamu baadhi ya maswali ya kawaida kabisa wanayoulizwa mawaziri bungeni huandakiwa majibu mapema kabisa kabla ya kusomwa bungeni.

Waziri au mabosi wanapoalikwa kuhojiwa jambo fulani katika interview za vyombo vya habari hupewa area of concentration

Ni viongozi wachache sana wenye uwezo wa "kumeza" takwimu, angalau wakuu wa idara ndio angalau wanakuwa na takwimu

Ikumbukwe pia kwamba hata mgombea mmoja wa urais alituambia Sadam alikuwa rais wa Kuwait. Hata katika mikutano mbalimbali kuna kiongozi alihutubia kwamba awamu ya kwanza ilipoanza bei ya sukari ilikuwa 5000. Mambo ambayo sio kweli. Tukamezea kwa kuna tunaamini kuna kupitia

Hiyo busara itumike viongozi wakubwa wanapowahoji viongozi wa chini hasa mbele ya majukwaa



Kuwatumbua wakurugenzi wasiojielewa kama hao ni sawa, inawezekanaje mkurugenzi ashindwe kuwa na takwimu kichwani ,mbona Meya kaweza kujibu? Nafasi walizopewa ni kubwa kupita uwezo wao waache wawapishe WANAOWEZA!!
 
Naomba kuuliza hivi katika mataifa ya watu walioendelea na kustaarabika, kiongozi unaweza kufanya maamuzi ya kuumiza hisia za wasaidizi wako hadharani na raia wakakushangilia?

Namba wenye majibu wanisaidie.
Tatizo huku ni elimu ndogo na ushabiki....
 
Back
Top Bottom