Nimeshamwambia jamaa, labda tuanze kuandaa kabisa michango ya kumpeleka Nairobi, maana ndio kimbilio pekee, je watu watatoa maana kila mtu na kismati chakeNaona Mayalla umejitoa mhanga...mimi kazi yangu kukuombea tu watu wasiojulikana wasikufuatilie...
Umeweka ujumbe mzito katikati ya mizaha.
Naomba ieleweke kwamba sitetei wakurugenzi wa Bukoba kutumbuliwa kwa sababu sababu za kutenguliwa kwao sizifahamu.
Hoja yangu itajikita jinsi Rais Magufuli,naweza kusema navyowapelekesha viongozi majukwaani kwa maswali ambayo yanahitaji Takwimu ambazo mda mwingine kiongozi anaweza kutokuwa nazo kichwani
Case Study iliyotokea Bukoba leo sio jambo la kuacha lipite.
Kwa wasiofahamu baadhi ya maswali ya kawaida kabisa wanayoulizwa mawaziri bungeni huandakiwa majibu mapema kabisa kabla ya kusomwa bungeni.
Waziri au mabosi wanapoalikwa kuhojiwa jambo fulani katika interview za vyombo vya habari hupewa area of concentration
Ni viongozi wachache sana wenye uwezo wa "kumeza" takwimu, angalau wakuu wa idara ndio angalau wanakuwa na takwimu
Ikumbukwe pia kwamba hata mgombea mmoja wa urais alituambia Sadam alikuwa rais wa Kuwait. Hata katika mikutano mbalimbali kuna kiongozi alihutubia kwamba awamu ya kwanza ilipoanza bei ya sukari ilikuwa 5000. Mambo ambayo sio kweli. Tukamezea kwa kuna tunaamini kuna kupitia
Hiyo busara itumike viongozi wakubwa wanapowahoji viongozi wa chini hasa mbele ya majukwaa
Ndio maana zile semina elekeza zilikuwa na manufaa makubwa sana kwa wake waliokuwa serious kupenda kujifunza kuhusu utendaji wa kila siku hususan unapokuwa umepewa dhamana ya kusimamia Idara au Taasisi, wengine unakuta hawajawahi kufanya kazi za kiutawala kuweza kuwafanya kuwa wafuatiliaji wa KEY ISSUES hususani barabara, afya, elimu na fedha kwa ujumla, kwa hiyo kwa mtu kuwa vizuri katika idara hiyo anatakiwa binafsi awena strategics za kufuatilia hivyo vipengele.Bwana Pascali. Swali aliloulizwa yule mama mara tatu mfululizo tena kwa kuonywa juu yabmajibu yake kwa Rais si swali baya kwa MKURUGENZI.
Haiwezekani mkurugenzi asijue ameletewa pesa kiasi gani kwa ajili ya BARABARA na akiba iliyopo ni kiasi gani.
Mkurugenzi anatakiwa afahamu akiba ya pesa zote alizonazo kila siku. Anatakiwa afahamu mapato na matumizi on daily basis.
Tatizo ni kuteua wakurugenzi ambao hawajawahi fanya kazi serikalini hivyo kutijua nini cha kufanya ofisini. Badala yake anataka mhasibu ndiye amsemee kwa bosi wake kwamba kuna pesa kiasi gani.
Isitoshe. Pesa za halmashauri hazipo kwenye mkundi mengi. Sana sana ni pesa ya barabara. Maji. Afya. Makusanyo ya ndani na miradi mingineyo ya hapa na pale.
Ashitakiwe huyukuna kiongozi alihutubia kwamba awamu ya kwanza ilipoanza bei ya sukari ilikuwa 5000
Ni ushenzi sana. DED huwezi kujieleza wakati wewe ndo key player hata meya anakuzidi? then unajitapa wewe ni kichwa, mtaalamu, really?TATIZO HAWAJUI KUJIELEZA..MBONA MAMEYOR WAMEWAZIDI
Wanabodi,
Kwanza naomba kukiri kuunga mkono kwa dhati, juhudi zote na hatua zote zinazochukuliwa na rais Magufuli katika vita dhidi ya rushwa, ufisadi, wizi wa rasilimali zetu na kusimamia uwajibikaji, ila katika utekelezaji wa juhudi hizo, sometimes kunatokea hapa na pale utekelezaji huo ukafanywa ndivyo sivyo, yaani doing the right thing, and the right time, but not doing it right. Kwa vile rais Magufuli, licha ya kuwa ni mtu anayeitwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, a human being, anaweza kufanya makosa ya kibinaadamu, lakini pia yeye ni taasisi inayoitwa Presidential Institution, taasisi hii ni purported to be perfect, haiwezi kukosea, hivyo rais Magufuli anategemewa kuwa perfect by doing the right thing, at the right time and do it right!. Makosa yoyote madodo madogo ya kibinaadamu, yanaweza kuwa tolerated yakifanywa na mtu mwingine yoyote, but not our president.
Angalia kilichofanyika hapa.
https://www.instagram.com/p/BbKBCKpnqK0/
Isn't This Bullying and Intimidation?.
Kwa maoni yangu, this is bullying na intimidation. Kwa rais Magufuli yeye binafsi is very good in numbers, actually I think he is genius kwenye kutunza kumbukumbu za numbers za takwimu, namkumbuka jinsi alipokuwa waziri wa mifugo, kichwani kwake, alikuwa na idadi ya ng'ombe, mbuzi, tena nikasikia kuwa ana hadi idadi ya samaki wetu. Alipokuwa waziri wa ujenzi, alikuwa na figures za urefu wa barabara zote za Tanroad na zimejengwa kwa kiasi gani. Then rais wetu asitegemee kila kiongozi wa umma, atakuwa mzuri kama yeye kwa kukurupushwa tuu na kuulizwa figures, alafu ajibu kutoka kichwani.
Is This Fair?, Huu Sio Udhalilishaji?.
This is not fair, hii sii haki, hii ni some sort of intimidation na udhalilishaji wa kiongozi wa umma mbele ya public ya watu. Hizi intimidations niliwahi kuzizungumza hapa. Kusema ukweli, kuna vitu rais wetu huwa anavisema, havikupaswa kusemwa na rais, na kuna vitu anavifanya, havikupaswa kufanywa na rais, kama wasaidizi wake mpo, na mnaona, na imejiridhisha he is doing the right thing, hivyo wote tuendelee kumshangilia tuu rais wetu, kwa baadhi yetu sisi ambao ni wakweli daima, tunakua hatujitendei haki nafsi zetu, hivyo mwisho wa uwezo wetu ni kusema tuu, kwa sababu hizi bullying na intimidations kwenye madogo zikiachwa, mbele ya safari tutakushuhudia makubwa Zaidi, tukidhani ndio kumsaidia rais wetu kumbe tunamchoresha!.
Tumbua Tumbua, Ziara za Kushutukiza na Utoaji Nje Siri za Serikali.
Niliwahi kupinga utekelezaji wa baadhi ya Tumbua tumbua, na kulalamikia double standards. Kwenye ziara za kushtukiza, nikasema ni intimidating, hivyo kutajenga nidhamu ya woga, lakini pia nikapinga hii ya rais kusema chochote hata vitu ambavyo hakupaswa kusema kama disclosure of tapping telephone conversations, au kuwaanika secret agents etc, nilishauri
Marais Wengine Hufanya Vipi?.
Nikiwa ripota wa newsroom, nimewahi kushiriki ziara nyingi za rais za ndani ya nchi na nje ya nchi. Wakati rais akifanya ziara popote, wahusika wote watakaohusiana na ziara hiyo huarifiwa. Rais akiishawasili hufanyiwa briefing, na kila jioni hufanya postmortem, hivyo kuna mambo mengine ni mambo ya ndani kuuliza kule kwenye briefings, na sio kila kitu kuuliza mbele ya kadamnasi ya watu, huu ni udhalilishaji na kuaibishana.
A Way Forward.
Kwa vile rais wetu pia ni binadamu, naendelea kuwasisitiza wale wasaidizi wake, waendelee kumsaidia rais wetu, kutenganisha the two personalities, kati ya mtu anayeitwa Dr John Pombe Joseph Magufuli, na Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Dr. Magufuli anaweza kuwaza lolote, kufanya lolote popote, au anaweza kusema chochote popote, lakini Rais Magufuli, hawezi kufanya lolote or kusema chochote, he got to do only the right thing at the right time and do it right!.
Namtakia ziara njema.
Paskali
Hapa umesomeka mkuu, na si kwa mtindo wa kukariri kama madent...!!Mkuu Paschal hao wakurugenzi kuna taarifa kuwa walikuwa wanafanyakazi kwa kushirikiana wa madiwani wa Chadema bila kubaguana, tatizo mzee hataki kuona watu waccm wanaelewana na wapinzani, mkuu umewahi kuona maswali kama hayo ameulizwa Bashite, Ally Happy, Mnyeti, Gumbo? hawa walikuwa wanatafutwa kwa muda mrefu, Mkurugenzi anawakuu wa idara kuna Engineer wa barabara kwa nini asiulizwe yeye?
hao 4 uliowataja....baada ya awamu hii kumaliza muda wake itabidi watafute nchi ya kuishi!Mkuu Paschal hao wakurugenzi kuna taarifa kuwa walikuwa wanafanyakazi kwa kushirikiana wa madiwani wa Chadema bila kubaguana, tatizo mzee hataki kuona watu waccm wanaelewana na wapinzani, mkuu umewahi kuona maswali kama hayo ameulizwa Bashite, Ally Happy, Mnyeti, Gumbo? hawa walikuwa wanatafutwa kwa muda mrefu, Mkurugenzi anawakuu wa idara kuna Engineer wa barabara kwa nini asiulizwe yeye?