Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?

Ni ushenzi sana. DED huwezi kujieleza wakati wewe ndo key player hata meya anakuzidi? then unajitapa wewe ni kichwa, mtaalamu, really?
Huyo DED atakuwa wa chadema...juzi wakati wanateuliwa tuliwambia waache kuteuwana makada..
 
Hakuna haja ya kupoteza fedha za umma kufundisha watu majukumu yao...wakati wanateuliwa wana fursa ya kujipima na kutambua kuwa kama wataweza kasi hii au la.
Hakuna sehemu ya kusomea ukurugenzi mkuu!!
 
Jingalao nakuunga mkono kwa asilimia 100% . Kwa hili la Mkurugenzi kutojua kiasi kilichoingia huku akiwa pia signatory Ni ujinga mkubwa na ni indicator kubwa kuwa haijui JD yake.
 
Huyu Mama anasimamia;
Afya,
Elimu Sec,
Elimu Msingi,
Utawala,
Ardhi,
Kilimo,
Maji,
Mifugo,
Uhandisi Majengo,
Uhandisi Barabara,
Utamaduni,
Mazingira,
Fedha na Uchumi,
Mipango,
Maliasili, nk

Je anatakiwa kujua Kila Fungu lililoelekezwa humo??
Anatakiw kujua kama sala...anatakiwa kumjua mtumishi mmoja mmoja.
Kwa maoni yako tukimuuliza DMO kwa nini kituo flani hakitoi huduma flani ya afya ataanza kusema nina vituo 60 vya kutolea huduma kwa hiyo sijakariri??Siku mkuu wa hospitali akiulizwa umeletewa kiasi gani fedha za dawa atajibu mpaka niongee na mfamasia??Huo ni upuuzi uliokuweko huko nyuma sasa ni wakati wa kazi tu.
 


Kuwatumbua wakurugenzi wasiojielewa kama hao ni sawa, inawezekanaje mkurugenzi ashindwe kuwa na takwimu kichwani ,mbona Meya kaweza kujibu? Nafasi walizopewa ni kubwa kupita uwezo wao waache wawapishe WANAOWEZA!!
 
Naomba kuuliza hivi katika mataifa ya watu walioendelea na kustaarabika, kiongozi unaweza kufanya maamuzi ya kuumiza hisia za wasaidizi wako hadharani na raia wakakushangilia?

Namba wenye majibu wanisaidie.
Tatizo huku ni elimu ndogo na ushabiki....
 
Suala la fedha unazosimamia kila siku sio la kitakwimu na information unayotakiwa uwe nayo at your finger tips hata Kama sio exactly lakini kusema hujui kabisa ni uzembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…