Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?

Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?

DED anapaswa kuwa na full informations za hamlashauri yake, lakini pia siungi mkono ishu ya kuwadhalilisha watumishibwa umma kiasi hicho. Lazima watu waandaliwe ili wajiandae kutoa ripoti kwa mkuu.
Ulitaka waandaliwe nini hasa ?
 
Paskal wewe ni Mwandishi mahiri, jee unakubaliana na zile data za kilometa, idadi ya ng'ombe au samaki?
Kaka zile zilikuwa fix mtupu!
 
ila uyu mzee jamani hata chembe ya ubinadamu hana? kama yeye amezoea kucrem madata alitaka mama wa watu acrem ili akosee amuumbue? poleni sna mnaofanya kazi na mshamba uyu kujiona perfect mungu mtu anataka kusujudiwa as if nchi ni Mali yake mbona Mara kibao anakoseaga au siyo yeye alisema fent Ford, kapata nini baada yakumdhalilisha mama wa watu
 
Bwana Pascali. Swali aliloulizwa yule mama mara tatu mfululizo tena kwa kuonywa juu yabmajibu yake kwa Rais si swali baya kwa MKURUGENZI.

Haiwezekani mkurugenzi asijue ameletewa pesa kiasi gani kwa ajili ya BARABARA na akiba iliyopo ni kiasi gani.

Mkurugenzi anatakiwa afahamu akiba ya pesa zote alizonazo kila siku. Anatakiwa afahamu mapato na matumizi on daily basis.

Tatizo ni kuteua wakurugenzi ambao hawajawahi fanya kazi serikalini hivyo kutijua nini cha kufanya ofisini. Badala yake anataka mhasibu ndiye amsemee kwa bosi wake kwamba kuna pesa kiasi gani.

Isitoshe. Pesa za halmashauri hazipo kwenye mkundi mengi. Sana sana ni pesa ya barabara. Maji. Afya. Makusanyo ya ndani na miradi mingineyo ya hapa na pale.
Hizo kazi za kujua takwimu on daily basis za Pesa kuingia na kutoka ni kazi ya Mweka Hazina.
 
Mkuu Paschal hao wakurugenzi kuna taarifa kuwa walikuwa wanafanyakazi kwa kushirikiana wa madiwani wa Chadema bila kubaguana, tatizo mzee hataki kuona watu waccm wanaelewana na wapinzani, mkuu umewahi kuona maswali kama hayo ameulizwa Bashite, Ally Happy, Mnyeti, Gumbo? hawa walikuwa wanatafutwa kwa muda mrefu, Mkurugenzi anawakuu wa idara kuna Engineer wa barabara kwa nini asiulizwe yeye?
gambo alikula za uso arusha aliitwa mpumbavu baada ya wateja kutokufika
 
bado sijaelewa sababu za msingi za kuuliza maswali, ikiwa majibu yanafahamika wazi! Kwa upeo wangu nilidhani pesa zimeliwa au zimepotezwa ktk mazingira ya ajabu, lkn baada ya kumsikiliza mstahiki meya , ni wazi pesa zipo au zimetumika ktk kile kilichokusudiwa what was the issue on the pulpit??

Please, naomba tufahamishame what was the aim na objective ya maswali ya kuhusiana na pesa za mfuko wa Bara Bara !

Na swala la pili je nini majukumu ya Mkurugenzi wa manispaa?

a5e11f9bfde3f3c01a610401e693bae2.jpg


I start questioning the motive behind the questioning ? Ni kukosa kujua takwimu au zaidi ya tunachokiona na kukisikia?
 
Hapa kazi tu.

Wakurugenzi hao wamejidhalilisha wenyewe,Halmashauri na mamlaka ya uteuzi.

Katika muktadha wa ziara ya kiongozi mkuu katika eneo lako haitarajiwi ukakosa data zote muhimu au maeneo mahsusi ya miradi iliyoletewa fedha na Serikali kuu.

DED kama accounting officer ana wajibu wa kujua kila senti iingiayo na kutoka halmashauri kwa kichwa kwani ni kazi yake ya kila siku na ni maswali anayoyajibu kwa wawakilishi wa wananchi au wananchi moja kwa moja.

Isitoshe mkurugenzi ana vikao vya kila juma au kila siku au kila mwezi vinavyombrief kuhusu maswala ya miradi ya maendeleo na fedha zinazotarajiwa kupatikana au zilizopatikana kutoka vyanzo vyote.yaani kuhusu fedha ya miradi kwa mkurugenzi ni sawa na sala ya baba yetu na muumini wa kikiristu.

Unapokuwa na mkurugenzi asitefahamu ni kiasi gani cha fedha za road fund zimefika kwenye halmashauri yake hutegemei kama ataweza kusimamia mradi wa barabara husika na mambo ndipo yanapokwamia na lawama au matusi yatarudi kwa mh Rais.

DED kama accounting officer aka afisa masuhuri wa halmashauri huandikiwa kwa barua kiasi cha fedha za mradi zinazoingia halmashauri sometimes days or weeks before disbursement ya hizo funds.

DED hupelekewa na mweka hazina statement au taarifa ya fedha yoyote inayoingia halmashauri.
Pia fedha yoyote inayoingia halmashauri hujadilowa kwenye vikao vya kamati za mipango na fedha na hatimaye baraz zima la madiwani ambalo katibu wake ni DED.

Kwa maoni yangu hakuna excuse ya DED kushindwa kujua figure ya fedha nyingi za mradi wa barabara zaidi ya kiwango kikuu cha uzembe.

Kama DED hajui ni kiasi gani cha fedha za mradi wa road fund ambayo ni nyingi how come anaweza kujua deni au fedha ya mtumishi(say nauli ya likizo) kama mdogo mfano mwalimu wa shule ya msingi aliyeko kwenye halmashauri yake???

Wakurugenzi hawa waneonesha kiwango kikubwa cha irresponsibility na wamestahili adhabu waliyopata.

Hilo ni funzo kwetu sote especially watumishi wa umma.

JPM ni no nonesense President, every subordinate must have known him better and therefore he/she should be super prepared .

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

You are genius
 
Mtu msinga tu ndio ata-support huu ujinga,hii inaonyesha vipi raisi wetu asivyo mstaarabu,Mkuu wa mkoa wa Daresalam nae ana tabia kama hii..

Raisi anataka kuwafanya watanzania wawe waoga,lakini raisi anatakiwa afahamu kuwa taifa lenye wananchi wenye nidhamu ya woga ni taifa dhaifu..

Kwakweli hii ni aibu kuwa na raisi kama huyu kwa nchi inayosifika kuwa na watu wastaarabu..
 
Mungu wa tanzania, anamtisha mama wa watu eti "usinijbu mimi hivyo!!!" Kakasirika kisa mama ana comfidence

Duh!! Anapenda kuabudiwa sana huyu kenge!!!

Kweli zama zimebadilika, sio kila homa ni malaria
 
We paskali tena ukiwa verified membe of jamii forum haogopi kufuatwa. Haya yote wanayajua, wanajua protokali jinsi gani mambo yanatakiwa yafanyike, lakini kama mkuu wa kaya hataki kuwasikiliza je wamsaidie vipi, au unataka wamshikie mtutu halafu waishie kupotezwa, tuache kama yalivyo, then majibu yatapatikana, but this is the REAL personality of our Presidaa
Paskali sio muoga katika kusema ukweli.
Kwi kwi kwi!
 
bado sijaelewa sababu za msingi za kuuliza maswali, ikiwa majibu yanafahamika wazi! Kwa upeo wangu nilidhani pesa zimeliwa au zimepotezwa ktk mazingira ya ajabu, lkn baada ya kumsikiliza mstahiki meya , ni wazi pesa zipo au zimetumika ktk kile kilichokusudiwa what was the issue on the pulpit??

Please, naomba tufahamishame what was the aim na objective ya maswali ya kuhusiana na pesa za mfuko wa Bara Bara !

Na swala la pili je nini majukumu ya Mkurugenzi wa manispaa?

a5e11f9bfde3f3c01a610401e693bae2.jpg


I start questioning the motive behind the questioning ? Ni kukosa kujua takwimu au zaidi ya tunachokiona na kukisikia?
Motive ya maswali sijui.

Majukumu ya Mkurugenzi ni pamoja na KUSIMAMIA MAPATO NA MATUMIZI ya halmashauri.

Sasa unasimamiaje matumizi kama hujui mapato. Maana yake hajui majukumu yake.
 
Hapa kazi tu.

Wakurugenzi hao wamejidhalilisha wenyewe,Halmashauri na mamlaka ya uteuzi.

Katika muktadha wa ziara ya kiongozi mkuu katika eneo lako haitarajiwi ukakosa data zote muhimu au maeneo mahsusi ya miradi iliyoletewa fedha na Serikali kuu.

DED kama accounting officer ana wajibu wa kujua kila senti iingiayo na kutoka halmashauri kwa kichwa kwani ni kazi yake ya kila siku na ni maswali anayoyajibu kwa wawakilishi wa wananchi au wananchi moja kwa moja.

Isitoshe mkurugenzi ana vikao vya kila juma au kila siku au kila mwezi vinavyombrief kuhusu maswala ya miradi ya maendeleo na fedha zinazotarajiwa kupatikana au zilizopatikana kutoka vyanzo vyote.yaani kuhusu fedha ya miradi kwa mkurugenzi ni sawa na sala ya baba yetu na muumini wa kikiristu.

Unapokuwa na mkurugenzi asitefahamu ni kiasi gani cha fedha za road fund zimefika kwenye halmashauri yake hutegemei kama ataweza kusimamia mradi wa barabara husika na mambo ndipo yanapokwamia na lawama au matusi yatarudi kwa mh Rais.

DED kama accounting officer aka afisa masuhuri wa halmashauri huandikiwa kwa barua kiasi cha fedha za mradi zinazoingia halmashauri sometimes days or weeks before disbursement ya hizo funds.

DED hupelekewa na mweka hazina statement au taarifa ya fedha yoyote inayoingia halmashauri.
Pia fedha yoyote inayoingia halmashauri hujadilowa kwenye vikao vya kamati za mipango na fedha na hatimaye baraz zima la madiwani ambalo katibu wake ni DED.

Kwa maoni yangu hakuna excuse ya DED kushindwa kujua figure ya fedha nyingi za mradi wa barabara zaidi ya kiwango kikuu cha uzembe.

Kama DED hajui ni kiasi gani cha fedha za mradi wa road fund ambayo ni nyingi how come anaweza kujua deni au fedha ya mtumishi(say nauli ya likizo) kama mdogo mfano mwalimu wa shule ya msingi aliyeko kwenye halmashauri yake???

Wakurugenzi hawa waneonesha kiwango kikubwa cha irresponsibility na wamestahili adhabu waliyopata.

Hilo ni funzo kwetu sote especially watumishi wa umma.

JPM ni no nonesense President, every subordinate must have known him better and therefore he/she should be super prepared .

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Tulikosea kuteua makada badala ya watu wenye taaluma
 
Siyo fair ila nilazma viongozi watambue nyakati zimebadilika.. Maraisi wote waliopita hakuna aliyefanya hivi na mambo yakawa Mabaya mno

Muacheni Magufuli bhana tunaeza kufika Pahala salama siku za mbeleni
 
Back
Top Bottom