jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Naona katekisa umekuja kuweka msisimtizo..Upo hapa unalalamika michango ya Jumuiya ambayo hugawanywa kila kaya let's say itoe 25,000/= siyo wewe peke yako na hulazimishwi kuchanga but wakati huo huo una wanao unawalipia school fees 2 millions na wapo watatu na ada hata ipandishwe vipi hulalamiki unalipa ila wakati huo huo unalalamikia kuendeleza pale unapoenda kumuomba Mungu ambaye unaamini anawalinda huko shuleni awasaidie wanao kimasomo halafu unajiita muumini?
Siku wakifeli lawama kwa Mungu ooh why God why God hapo tena yoote unayasahau,watu mnapenda vitu smooth sana hii imani wapo watu wameifia,Mtume Petro amesulubishwa kichwa chini miguu juu wapo waliotumbukizwwa kwenye mapipa ya mafuta yanayochemka lakini Mkristo wa leo unalalamika kutoa 5K mchango wa kupaka Kanisa rangi mimi natamani ifike siku Kanisa liseme yeyote asiyeweza kuziishi sheria za Mungu na Kanisa sawasawa huyo ametengwa,sijisifii ila mimi natoa sana michango na toka nianze kutoa hakuna siku nimekosa kula,kufanya maendeleo yangu binafsi au kuweka akiba ya kutosha.
Mkiambiwa toeni Zaka hamtaki unadhani kwa wingi Makanisa ya Kikatoliki yanaojaza kila mmoja angetoa Zaka kikamilifu kuna ambaye angeombwa atoe mchango wa aina yoyote?
#MaendeleoHayanaChama
Sent using Jamii Forums mobile app