Je, huu ni wakati sahihi wa Rais Magufuli kufunga balozi za mabeberu, tubaki na balozi tu ambazo sio za kibeberu?

Je, huu ni wakati sahihi wa Rais Magufuli kufunga balozi za mabeberu, tubaki na balozi tu ambazo sio za kibeberu?

Tanzania kwa miaka yote ni nchi ambayo mambo yetu low profile hatuna ugomvi na mtu na kupendwa sehemu nyingi tu maana hatujawahi kutawala vichwa vya habari kwa ubaya.

Ila kwa sasa nadhani kama tumechoka hivi kiko tunachotafuta na tutakipata. Kuna wakati nadhani sisi ni muhimu sana hatuhitaji mtu.

Tuache mabeberu nadhani hata jirani zetu wa karibu wanatuangalia na jicho la mashaka. Hivi tutagombana na wangapi? hii nchi haina washauri?

CCM hawana vikao vyao vya ndani na kupima haya kisiasa na kiuchumi na kufanya maamuzi sahihi? au kuna uwoga umetawala watu.

Siku unajigamba tajiri siku unaomba usamehewe deni, siku hakuna corona, siku tuanze kujifukiza siku 3.
Acha uwoga! Wewe umeona hapa tumeanzisha ugomvi na Nani?
 
Hana ubavu wowote wa kufunga balozi yeyote ya mabeberu, labda afunge ya Commoro, Madagascar na Usherisheri
 
Swala la wao kuleta Virusi vikali ili tufe zaidi, wanaweza kweli hao watu Kwa vile Sisi na Nchi nyingi za Africa hatuna mifumo imara ya kuzui njama hizo za Kisayansi

Acheni kupotosha! Ugonjwa huu, ni kama maji ya bwawa, tunayatumia wote. Haiwezenani ikamwagwa sumu upande wetu, wakati maji haya haya yanazunguka bwawa zima!
Ndiyo maana, wanataka tushirikiane Dunia nzima kupambana nao!
 
Mtu akutukane tusi lolote duniani atakuwa hajakutukana kuliko atakayekwita wewe ni CCM atakuwa amekutukana kwelikweli kwa kuwa itakuwa na maana wewe ni mjinga, juha, mpumbavu, hovyo kama wao.

Ona CCM huyu anamshauri CCM mwenzake afunge Balozi za mabeberu kwa sababu wanazuia watalii kuja nchini ili tukose mapato na kwao Covid-19 inazidi kuongezeka kila siku na haitashangaza ushauri huu kukubalika maana ni wao kwa wao.

Mjukuu wangu wa Chekechea angeshauri Balozi zetu kwenye nchi za mabeberu zifungwe na wafanyakazi wabaki hukohuko bila mshahara wasituletee ugonjwa mpaka watakapofukizwa.

Balozi za mabeberu zibaki tu maana zinatuletea pesa za kigeni zinazoletwa kugharamia uendeshaji wa Balozi na kuwataka Mabalozi wapeleke shukrani za dhati kwa Serikali zao kwa kuzuia watu wao kuja huku kuwaletea Watanzania gonjwa ambalo sasa halipo.

Kuhusu vita vya uchumi mnavyodai vinaendelezwa na mabeberu dhidi yetu, huyu anasahau kuwa kwa juhudi za Rais wao chuma, mwamba, bulldozer, nchi yetu ni donor country na Miradi yote inatekelezwa kwa fedha za ndani.

Banian mbaya, kiatu chake dawa!
 
Mtu akutukane tusi lolote duniani atakuwa hajakutukana kuliko atakayekwita wewe ni CCM atakuwa amekutukana kwelikweli kwa kuwa atakuwa na maana wewe ni mjinga, juha, mpumbavu nk. CCM huyu anamshauri CCM mwenzake afunge Balozi za mabeberu kwa sababu wanazuia watalii wasije nchini ili tukose mapato na kwao Covid-19 inazidi kupanga na haitashangaza ushauri huu ukijubalika maana na wao kuwa wao. Mjukuu wangu wa Chekechea angeshauri Balozi zetu kwenye nchi za mabeberu zifungwe na wafanyakazi wabaki hukohuko bila mshahara wasituletee ugonjwa mpaka watakapofukizwa. Balozi za mabeberu zibaki tu maana zinatuletea pesa za kigeni zinazoletwa kugharamia uendeshaji wa Balozi na kuwataka Mabalozi wapeleke shukrani za dhati kwa Serikali zao kwa kuzuia watu wao kuja huku kuwaletea Watanzania gonjwa ambalo sasa halipo.
Codes cracker
 
Twende na dunia kama tulivyokuwa tukienda tangu uhuru.
Tumechepuka na matokeo yake dunia inaanza kutuacha halafu tunalalamika.
 
Acha uwoga! Wewe umeona hapa tumeanzisha ugomvi na Nani?
Taja nchi moja duniani wanaodharau huu ugonjwa kama Tanzania? ndio maana jana cartoon imechorwa dunia nzima wanaimba kwaya Tanzania wanacheza singeli. Hizi message hazifutiki siku utakumbushwa tu. Naandika hii kuna mtu wa karibu yuko ICU anapigania maisha yake.
 
Wewe unataka tuiheshimu korona? Tutaidharau kama tunavyowadharau walioileta ukiwepo na wewe!

Korona ipo, ila kiwango cha kufikia maambukizi na vifo vingi kama huko unakokuabudu, haitafika na ifikapo nusu ya mwezi Huu wa pili, Tutaitangaxia Dunia tena kwamba, Mungu kaingilia Kati tena, hatuna Corona inayoitwa wimbi la pili la maambukizi duniani

Pole yake aliyeko ICU, Na Mungu Ampe nguvu na uponyaji
 
Pole yake aliyeko ICU, Na Mungu Ampe nguvu na uponyaj

Wewe unataka tuiheshimu korona? Tutaidharau kama tunavyowadharau walioileta ukiwepo na wewe!

Korona ipo, ila kiwango cha kufikia maambukizi na vifo vingi kama huko unakokuabudu, haitafika na ifikapo nusu ya mwezi Huu wa pili, Tutaitangaxia Dunia tena kwamba, Mungu kaingilia Kati tena, hatuna Corona inayoitwa wimbi la pili la maambukizi duniani

Pole yake aliyeko ICU, Na Mungu Ampe nguvu na uponyaji
Nimejifunza kitu kuna Miungu siku hizi na Tanzania tuna wa kwetu anatupenda sana.
 
Back
Top Bottom