Japokuwa umeandika pasipo mpangilio lakini mimi nimekuelewa. Umesema kijana wako amefeli somo moja katika mtihani wa kidato cha sita na hili linamnyima fursa ya kuendelea mwaka wa Tatu katika masomo yake ya Diploma maalum hivyo unaomba apewe upendeleo wa kuendelea mbele hivyo hivyo!
Upande wa pili umesema kijana wako ana juhudi kubwa wana ya kusoma lakini ana ugonjwa wa kusahau na yuko kwenye dawa.
Ushauri wangu ni huu;
-Huo upendeleo haupo!
-Kama anaruhusiwa kurudia mwaka ajipange kurudia tu mwaka.
-Huenda hii fani ya kusoma soma, kuelewa, kukumbuka na kuja kufundisha hamfai kijana wako (kwa hali alinayo), tafakari tofauti na fikiria fani nyingine ambayo itakuwa bora zaidi kwake.