Right Marker
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 194
- 625
Katika utafiti wangu nimegundua kuwa kwenye maisha ya kujitafuta/utafutaji/kufanya uamuzi, watu wamegawanyika katika makundi matatu.
1. Watu ambao wana kipawa cha kugundua hasara/madhara kabla ya kufanya uamuzi....
Hawa ni watu ambao wanapata majibu ya uamuzi kabla ya kufanya uamuzi. Kwa mfano kabla hakuanzisha biashara, kukopa hela, kununua bidhaa, au mali, tayari anagundua madhara/hasara kuwa akithubutu kujaribu atapigwa na kitu kizito kichwani. Haraka sana anabadili wazo.
2. Watu ambao wanagundua hasara/madhara baada ya kufanya uamuzi....
Hawa ni watu ambao majibu ya hasara huja wakati ambao tayari washafanya uamuzi. Mara nyingi watu hawa ni wale ambao hufanya uamuzi wa haraka sana, kwa mfano akishika hela anafanya matumizi ya haraka hata kama ni matumizi ya maana lakini hajui hasara yake, baadaye anagundua amepigwa na kitu kizito kichwani. Anaweza kununua gari la kutembelea halafu baadae anagundua kuwa gari halikuwa na maana kwake, kisha anauza kwa bei ya kutupa ili afanye jambo lingine.
3. Watu ambao hawagundui hasara/madhara yoyote hata baada ya kufanya uamuzi.....
Hawa ni watu ambao mpaka jambo linawafia mikononi bado haelewi alikosea wapi. Mpaka anafilisika hajui kosa lake lilikuwa wapi. Mara nyingi hukimbilia kuhusisha uchawi au imani potofu juu ya hasara anayoipata pasipo kujua alikosea wapi.
KARIBU TUSHIRIKI MJADALA:
(1) Je, wewe au rafiki yako upo/yupo kwenye kundi gani?
(2) Toa maoni/ushauri kwa kundi lolote kati ya makundi hayo.
(3) Kama una njia ya kumshauri mtu aboreshe au aondokane na kundi hilo, eleza.
RIGHT MARKER
Dar es salaam.