benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Kwani hatuna vijana wa kiume walioacha masomo kwa kusababishiwa na wazazi au walezi wao hata wakajikuta wamepotea mtaani?
Katika miji na majiji vijana wa kiume wanafanya kazi ya kukata nyasi za mifugo, kuuza kahawa kwenye mabirika, kusafisha vioo vya magari na wengine wapo kwa ajili ya kufanya kazi ya utwana ikiwemo kufungua mageti ya wakubwa.
Heri ya hao, lakini wapo waliokimbilia kwenye muungano wa vikundi hata wakabatizwa majina ya panya rodi na panya kalowa kazi yao ikiwa ni mapambano ya kutafuta mali kwa kukwepa bomba la bunduki ambalo huelekezwa kwao.
Vijana wengi wanaokosa elimu huwa wametengenezewa ajali za kushindwa kufikia ndoto zao kama ilivyo kwa Watoto wa kike ambao wao wamewekewa kivuli katikati ya jua.
Je nani awaseme vijana wa kiume ili kuja na dawa ya kuwasaidia? Tutakapoendelea na mpango wa kuwasaidia kundi la wasichana, ni wazi kuwa vijana wa kiume wanahitaji mpango maalumu wa kuwapatia elimu kwa waliokosa vinginevyo baada ya muda mfupi ujao tutakuwa na wasomi wengi wanawake kuliko wanaume ambao elimu inawatengenezea handaki la kuzama. Katika mambo mengine tuachie iwe hivyo, lakini mambo mengine muhimu, watoto wa kiume wasiachwe kwani watakuwa wanaandaliwa bomu wakati wasichana wakiandaliwa kivuli upande wa wavulana kwenye elimu watakuwa wamegubikwa blanketi jeusi.
Elimu yetu itazame pande zote ili kuweka msawazo, taasisi ziangalie kwa namna gani makundi haya mawili yanaweza kwenda pamoja kutimiza malengo ya nchi yetu.
Serikali ifanye tathimini ya kutosha kuhusu wasichana na wavulana katika mahitaji ya shule na malezi yao kuanzia hatua za awali bila kubagua. Kama shule za wasichana zimejengwa na zinaendelea kujengwa kila mkoa, kuna ubaya gani kuongelea shule za wavulana kwenye mikoa yote Tanzania ili tuanzishe kampeni ya ujenzi japo kwa kila kanda shule moja itakayoungana na shule zilizopo?
Hii inanikumbusha kauli aliyowahi kuitoa ndani ya Bunge wakati fulani Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu kwamba wanaume ni mbegu adimu inahitaji kutunzwa na kupaliliwa ili iwe imara.