ANT - NYONDENYONDE
Senior Member
- Jul 29, 2024
- 154
- 173
Swali, Je, huenda Freeman Mbowe akajitoa ili kulinda heshima kidogo aliyonayo au yuko tayari kubeba aibu kwa gharama ya chawa wake||
Taarifa za chinichini ni kwamba,
Mtia nia wa nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa Bwana Tundu Lissu ameshamaliza Uchaguzi tayari kinachosubiriwa kwa sasa ni wanachama ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu kupiga kura tu tarehe 21.01. 2025.
Watu wake wa karibu wanasema mtiania wao huyo huenda akashinda Uchaguzi huo kwa zaidi ya asilimia 70 ya kura zote zitakazopigwa kwani wanachama wa CHADEMA hasa wale walioduni sana kimaisha na kielimu ambao ni wengi wanaonesha kumuhitaji zaidi Tundu Lissu kwa sasa kuliko Freeman Mbowe kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.
Lissu anayeungwa mkono kwa karibu na makundi yote hasa BAWACHA, BAVICHA , BAZECHA pamoja na idadi kubwa ya wajumbe wa mkutano mkuu Kuna kila dalili atashinda kwa kishindo na KUWEKA rekodi mpya katika siasa za CHADEMA ngazi ya Taifa.
Pitia hapa pia KURA: Je, ni nani kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu anayefaa zaidi kuiongoza CHADEMA kwa Sasa?
Hata hivyo,Tundu Lissu anaonekana kupata nguvu zaidi kwa karibu kila siku tangu atangaze nia yake hiyo ya kutaka kumrithi Freeman Mbowe aliyehudumu kwa zaidi ya miaka 20 madarakani ambaye mpaka Sasa bado hajasema kama atagombea au laa.
Freeman Mbowe anayeonekana kuyapoteza kabisa malengo ya kuanzishwa kwa CHADEMA na kijiegemeza zaidi kwenye kutafuta kukubalika kwake na dola pamoja na Viongozi wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa CCM kuliko kwa Wafuasi na Wapenzi wa CHADEMA jambo hili linawakasirisha zaidi wanachama wa CHADEMA walio wengi kiasi Cha kutamani kubadili Mwenyekiti kwa gharama yeyote.
"Mbowe anakabiliwa na anguko Kali la imani toka kwa wapenzi na Wanachama wa CHADEMA ndio maana Lissu hata asipofanya kampeni yoyote sisi tutamchagua na nilazima" imeelezwa hivyo na kamanda mmoja toka Kilimanjaro jina tunalihifadhi,
Freeman Mbowe Mwenyekiti anayemaliza muda wake anakabiliwa na kosa la ukosefu wa Uaminifu na Uadilifu kwa wanachama na Wafuasi wa CHADEMA hasa baada ya kuonekana akiwa na ukaribu zaidi na Mwenyekiti wa Chama tawala kiasi Cha kupatiwa pesa kwa mamilioni ili apeleke kwenye makanisa pamoja na matumizi binafsi mathalani kwa Askofu Dkt Shoo alikopeleka zaidi ya Mil 150 za ununuzi wa gari pesa toka kwa Rais Samia ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM.