Tetesi: Je, huyu ndiye Mwenyekiti mpya wa CHADEMA ajaye?

Mika 20 sio hapa
 
Hata Lissu asiposhinda tayari amesaidia kutuonesha rangi halisi ya CDM, hawataaminika tena na wananchi na sijui 2025 watakuwa na lipi la kusema.
 
Mbowe akae pembeni tu upepo wa Lissu ni mkali sana
 
Siasa kama hizo Zina nguvu Kenya, Zanzibar na sehemu zifananazo ila sio Tanzania bara.
Siku zote watu uangalia kiongozi aliyopo juu wengine ufuata mzee hata hapa Tanzania inawezekana unakumbuka kwenye Msiba wa Mzee kibao kilichokua kinaenda kumtokea Waziri wa ulinzi Masauni Msibani wananchi walichachamaa Mbowe alifanya nini mzee watu uangalia msimamo wa kiongozi wao Mbowe hawezi kua mpinzani kwa siasa za Afrika
 
Nafkri hujanielewa, wewe una uhakika Gani watamchagua kutokana na siasa afanyazo, na si sababu nyingine labda kuchoka uongozi Mmoja wa muda mrefu?
Nime kuelewa vizuri kabisa; na hata sasa nakuelewa haya uliyo andika hapa.
Maana yake ni ile ile niliyo kupa mwanzo.
Bila kujali hao watakaomchagua watamchagua kwa sifa ipi, wewe unataka akisha chaguliwa tu, abadilike! Sasa hilo ndilo tatizo lenyewe. Kwa nini abadilike. Huoni kuwa huu utakuwa ni utapeli mkubwa, sawa na huu tunao ushuhudia leo hii kutoka kwa Samia Suluhu Hassan?
Wewe unataka viongozi laghai, wasio aminika kwa lolote walisemalo?
 
TL aliwahi kuwa Rais wa TLS!
Tuambieni kipindi hicho aliweza kufanya nini kuisaidia TLS,Leo anaomba kuwa mwenyekiti wa chama kikuu Cha upinzani?
Lissu alikuwa Rais wa TLS kwa kipindi kifupi sana tu ndiyo Magufuli akatuma wauaji wakampige risasi.
 
Chadema mna mambo. Mara mseme siye mara niyeye sasa tuwaeleweje sisi .?
 
Cc.Luca,Tlaattla na rafiki zao uwafikie ujumbe huu.
 
TL aliwahi kuwa Rais wa TLS!
Tuambieni kipindi hicho aliweza kufanya nini kuisaidia TLS,Leo anaomba kuwa mwenyekiti wa chama kikuu Cha upinzani?
Alikaa madarakani TLS kwa muda gani?
Hukumbuki kuwa wauaji walimjeruhi vibaya siku chache tu baada ya kuchaguliwa?
 
Kama kusema ukweli tu kunatosha basi kina Kiiza Besigye wangeshakuwa Marais, mimi nasema bado hujaelewa nilichomaanisha mkuu...
 
Unajua kuna kupigania haki na kuna mbinu za kupigania haki, wewe umezungumzia la kwanza, Mimi nimezungumzia la mwisho.

..kwanini tusipewe hizo haki mpaka kuwe na confrontation?

..kwanini watawala hawataki kuunda Tume huru, na kuandika katiba mpya mpaka kuwe na confrontation?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…