Je, ikitokea tukaachana na mwanamke mali tutagawana hali tuliwa hatukufunga ndoa?

Inawezekana pia But mwisho wa hiyo Nyumba itakuaje huko mbeleni? I mean watoto wamesha kua wakubwa tayari au jamaa kaoa kwingine na Mwanamke akaolewa kwingine.

Watarud Mahakaman waombe shaur la kuuza.

Sababu ya kutokuuza muda huu ni kuwa mali itagawanywa nusu kwa nusu na bado mwanaume atatunza watoto wake. Bora ipangishwe iendelee kupanda thaman.
Ikiuzwa sasa Baada ya miaka 2 hela ya nyumba itakuwa ishaisha.

Kuna mdogo wangu niliwah kumuajiri kwenye kibanda changu cha uwakala mwaka 2015 na 2016. Ameachana na muwewake. Hawakufunga ndoa.
Wana mtoto mmoja.

According na dogo. Kiwanja na nyumba yeye kachangia 70% na jamaa ni 30% ila mahakama imeamua nyumba iuzwe na madalali neutral na hela igawane.

Mill 45. Iko Kimara bunyokwa.
Jamaa kakataa. Anasema hela ndogo. Na anakaa kwa nyumba bado. Na bidada yuko kapanga.

Kwahiyo ni stress juu ya stress.
 
Hili la kumuachia mali mwanamke kisha wewe usonge mbele,inategemea na umri wa muhusika pia,

Imagine,mwanaume yupo kwenye 40-50s hapo inakua ngumu kuachia mali ili ukaanze upya.
 
Hili la kumuachia mali mwanamke kisha wewe usonge mbele,inategemea na umri wa muhusika pia,

Imagine,mwanaume yupo kwenye 40-50s hapo inakua ngumu kuachia mali ili ukaanze upya.
Imenitokea binafsi, nikawaachia mjengo na kila kitu, nikaondoka na corolla yangu 110, ilikuwa 2019 nikiwa na 40, sijafanikiwa saaana ila sipo vibaya, sasahivi tunalea watoto wetu kwa amani
 
Miaka 8, Ahahah nyie ni Bibi na Bwana wa kwenye Ngao ya Taifa kabisa. HUTOBOI CHIEF.
 
mkiishi kama mke na mume Kwa zaidi ya miaka 2 na jamii ikawaona na kiwachukulia hivyo mtakuwa mkichukuliwa nikama mke na mume (dhana ya ndoa).

kuhusu mali mlizochuma Kwa pamoja.
kila upande yaani mke na mume mnayo haki yakugawana KULINGANA na mchango mliochangia katika upatikanaji wa mali husika.
mwanaume atawajibika kutoa matunzo ya watoto na si mke.
NB: MALI SI YA WATOTO NI YA BABA NA MAMA
 
Ndoa za kikristo not Islam kwenye Uislamu hakuna upumbavu huu eti pasu kwa pasu
 
Ukiwa na mwanasheria mzuri utaruka viunzi vingi tu, huyo sio mkeo ni hawara technically
 
ndio mtagawana. Ndio kusudi la sheria ya ndoa kuweka hio kitu inayoitwa dhana ya ndoa. Lengo la kuweka kifungu cha kisheria cha dhana ya ndoa nikulinda haki za watu wawili wanaoishi Kwa pamoja kama mke na mume BILA kufunga ndoa Kwa miaka zaidi ya miwili pindi watakapo amua kutengana.

kwahio kutofunga ndoa hakuzuii kugawana mali mlizochuma Kwa pamoja kipindi chote mlichokuwa mkiishi kama mume na mke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…